Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » ZIFAHAMU DONDOO 5 TOKA KWA TOVUTI BORA TANZANIA ZA JINSI YA KUBORESHA BIASHARA YAKO

ZIFAHAMU DONDOO 5 TOKA KWA TOVUTI BORA TANZANIA ZA JINSI YA KUBORESHA BIASHARA YAKO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Ijumaa ya tarehe 27 januari mida ya jioni, makampuni na mashirika makubwa na madogo  pamoja na wafanya biashara mbali mbali Tanzania walikusanyika katika hotel ya  Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kushuudia utowaji wa tuzo za  Tanzania Leadership Awards 2016. Tuzo hizi za  heshima hutolewa kwa biashara  na wafanyabiashara bora nchini.

Katika hafla hiyo, ZoomTanzania, tovuti inayoongoza kwa matangazo ya biashara (kununua na kuuza)  nchini, ilinyakuwa tuza ya ' tovuti bora ya mwaka'. Hii ni mara ya pili kwa Kampuni hii ya kitanzania kupewa heshima kwa utaalamu wake wa mtandaoni, mwaka jana ilishinda tuzo ya kampuni bora ya biashara za mtandaoni.

Kutokuwa na uwepo wa biashara yako mtandaoni ni hatari kwa biashara yako


Kuna watumiaji wa internet zaidi ya milioni 17 nchini Tanzania, wafanya biashara zaidi na zaidi wanaanza kutambua  umuhimu wa kuwa na uwepo mtandaoni, wengi wao wameanzisha  tovuti zao ili kuweza kwenda sambamba na soko la mtandaoni linalokuwa kwa kasi

Hata hivyo, wengi wa wafanyabiashara hawana ufanisi wa kubadilisha watumiaji wa mitandao kuwa wateja.

Kwa bahati nzuri, kampuni ya ZoomTanzania inaelewa jinsi ya kutengeneza tovuti nzuri ya biashara itayowavutia  watanzania , kwa leo watakujuza dondoo 5 zitazo kusaidia kuboresha tovuti yako ya biashara mwaka huu.

1. Ni muhimu tovuti yako itumike kirahisi kwa kutumia simu za mikononi

Zaidi ya 67% ya Watanzania wanatumia simu za mikononi, na karibu 50% ya watumiaji wa internet hutumia  simu zao kutafuta  vitu mtandaoni . Kwa hivyo, kuwa na tovuti inayotumika kirahisi kwa kutumia simu za mikononi ni muhimu sana ili kupata wateja wanao tafuta vitu mtandaoni kutupitia simu zao
Kumbuka, kadri unavyo rahisisha upatikanaji wa tovuti yako ndivyo unavyoweza kubadilisha watumiaji kuwa wateja

2. Kurasa za tovuti yako zinapaswa kutoa ufumbuzi

Kama  ni mgahawa au kampuni ya ulinzi,  watu wanatembelea tovuti yako kwa sababu wanatafuta ufumbuzi. Hii ina maana kwamba, tovuti yako lazima iweke wazi jinsi biashara yako itawasaidia kutatua matatizo yao.

Hivyo, badala ya kusifia  biashara yako, unapaswa kutambua  na kuzingatia changamoto za wateja wako na kueleza jinsi gani unaweza kuwasaidia.

Kwa mfano, kama kampuni yako inatoa Huduma za matangazo ,basi Kurasa zako zisielezee tu jinsi gani Huduma zako ndio bora kuliko zingine zote badala yake, ni muhimu kuwajulisha wateja wako ni faida gani watapata kutangaza kupitia kampuni yako, kwa mfano ni idadi ya watu wangapi wataona matagazo yao.

3. Ni muhimu kufanya content marketing

Njia nyingine ya kutatua matatizo ya watumiaji wako na kuonyesha thamani yako na uaminifu kama biashara ni kuonyesha kwamba wewe ni mtaalam katika sekta yako. Njia moja kubwa ya kufanya hivyo ni kuwa na blog kwenye tovuti yako ambayo hutoa taarifa muhimu juu ya mada ambazo ni muhimu kwa wateja wako.

 Aidha, Njia za utafutaji kama Google uzingatia content marketing hivyo kufanya tovuti yako ionekane  juu endapo mteja atakuwa anatafuta kitu  katika sekta yako ya biashara ,

Hivyo, kwa mfano, kampuni ya vifaa vya ujenzi ambayo ina blog na makala kama 'Jinsi ya Kujenga Nyumba yako mwenyewe', 'Maswali 10 ya kumuuliza Mkandarasi kabla yakumuajiri ', na' Faida na hasara za kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ' itakuwa na uwezekano mkubwa kuonekena kwenye google search pale mtumiaji anapotafuta tovuti za sekta ya ujenzi

Bado hujaamini? Utafiti uliofanywa na Hubspot  ulionyesha kuwa biashara ambazo uweka kipaumbele matumizi ya blog hufurahia mara 13 zaidi ROI kuliko wafanyabiashara ambao hawana blog!

4. Tumia lugha inayofahamika vizuri na wateja wako

Kiswahili ni lugha maarufu zaidi katika mazingira rasmi na yasio rasmi nchini Tanzania, hata hivyo,  kwa baadhi ya biashara na sekta ni muhimu kuwasiliana kwa Kiingereza.

Kama we ni mfanya biashara wa sekta kama hii ni muhimu  kuwa na tovuti ya lugha mbili (Kiingereza na Kiswahili). Hii itakufanya uweze kufanya vizuri katika sekta yako inayotumia kiingereza na pia kuvutia watumiaji wa lugha ya kiswahili wanaotafuta huduma.


5.Tengeneza kurasa zitazo badilisha watumiaji kuwa wateja

Mwisho wa siku, lengo kuu la tovuti yako ni kupata wateja. Hivyo, iwe ni jinsi gani yakuwasiliana na biashara yako, kuweka apointimenti, au kujiunga na blog ya  biashara yako, kila ukurasa inapaswa kuwa na wito wa kuchukua hatua( call-to-action). Hii ni pamoja na:

•  Fomu za kujiunga ( sign up and subscribe )
•  Namba za simu na barua pepe kurahisisha mawasiliano
•  Tovuti iunganishwe na mitandao ya kijamii
•  Actionable buttons za kurahisisha kupakua materials za sales na fomu za matangazo

Mtumiaji hapaswi kupata shida kutafuta kitu katika tovuti yako. Jaribu kurahisisha na kuweka mambo wazo kadri uwezavyo

Pata matokeo unayoyataka

Kadri idadi ya watumiaji wa internet inavyoendelea kuongezeka nchini Tanzania, ndivyo watu zaidi na zaidi wavyozidi kutafuta bidhaa na huduma mtandaoni. Kwa bahati nzuri, dondoo hizi  5  zitarahisisha tovuti yako ipatikane kirahisi,  kufanya wateja wengi watumie tovuti yako na kufanya biashara yako iwe juu zaidi ya washindani wako.

Kama unataka biashara yako ionekane zaidi mtandaoni, Jifunze zaidi kuhusu ufumbuzi wa matangazo toka  ZoomTanzania bofya hapa.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa