Na Daudi Manongi-MAELEZO
Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa
Mashirika ya Umma na Mamlaka za udhibiti kuwa wabunifu na kutumia fursa
na rasilimali zilizopo nchini ili kuleta maendeleo chanya.
Amebainisha
hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa
kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa mpango wa
pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.
“Rai
yangu leo ni kwamba kwenye majadiliano yenu pendekezeni na kufanya
mashirika ya umma yawe endelevu,yapanuke zaidi na kuliongezea Taifa
mapato na ndio maana nafarijika sana kuona mkutano huu unajumuisha wadau
wote muhimu ili pamoja na kuweka mikakati ya namna mashirika ya umma ya
Tanzania yanavyoweza kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango wa
Maendeleo,”Alisema Majaliwa.
Akielezea
hali ya mashirika ya umma nchini,Waziri Mkuu amesema kuwa utegemezi wa
mashirika unaendelea kupungua na mchango na gawio kutoka kwenye
mashirika hayo unaendelea kuongezeka na kuhimiza kuongezeka kwa ubunifu
na matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo na kuongeza kati ya
mashirika 65 ya kibiashara,mashirika 8 yanaendeshwa kwa Ruzuku ya
Serikali,wakati mashirika 57 hayategemei ruzuku ya Serikali.
Ameagiza
kuboreshwa kwa mwongozo wa kupata wajumbe wa Bodi na kuwaagiza kuweka
mwongozo rasmi wa namna ya kupata wajumbe hawa kwani ni sehemu
inayolalalmikiwa sana na wananchi.
Amesema
kuwa wameyashirikisha mashirika ya umma kwenye utekelezaji wa mpango wa
maendeleo kwa sababu vipaumbele vya mpango wa pili wa maendeleo wa
Taifa wa miaka mitano ambayo ni ujenzi wa viwanda vya kuimarisha kasi ya
ukuaji wa uchumi,miradi mikubwa ya kielelezo na miradi wezeshi kwa
maendeleo ya viwanda ikiwemo barabara,reli,nishati,bandari maji na
mawasiliano.
Aidha
ameagiza kuondolewa kwa urasimu katika shughuli za mashirika ya umma
kwani unakwamisha uboreshaji na maendeleo ya mashirika ya umma.
Waziri
Mkuu pia ametoa rai kwa viongozi wote wa mashirika ya umma kutosaini
mikataba isiyo na tija kwa Taifa ambayo inapelekea kupata hasara kubwa
na kuhimiza mashirika haya kushirikiana na mashirika ya nje pamoja na
sekta binafsi ili kupata nguvu ya pamoja katika kukuza uchumi.
0 comments:
Post a Comment