Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAONYESHO YA KIMATAIFA YA TASWE YAANZA KWA KISHINDO UKUMBI WA CARDINAL RUGAMBWA OYSTERBAY - DAR

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA TASWE YAANZA KWA KISHINDO UKUMBI WA CARDINAL RUGAMBWA OYSTERBAY - DAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Maonyesho ya Kimataifa ya Ushirika wa akinamama wajasiliamali wa Tanzania (TASWE) yameanza kwa kishindo leo katika ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay. Akizungumza kwa juu ya maonyesho hayo, mwenyekiti na mwanzilishi wa Taswe Saccos, Bi Anna Matinde alisema "Maonyesho haya yamekuwa na hamasa kubwa wafanyabiashara na bidhaa kutoka Comorro, Afrika Mashariki na mikoa mbalimbali nchi zinapatikana hapa kwa wingi na kwa bei nafuu. "Tunawakaribisha wote mje mkutane na wafanyabiashara hawa pamoja na wadau wetu na kujionea bidhaa mbalimbali. Maonyesho yanaaza saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku", . Aliongeza Anna Matinde.
Mfanyabiashara kutoka Comorro, Siti Marahaba akiuza baadhi ya bidhaa zake katika maonyesho ya kimataifa ya Taswe
 Bi Sarah Abiudi akionyesha bidhaa za kiafrika zinazopatika katika maonyesho ya Taswe.
 Bi. Arafa Awadhi Mfanyabiasha mwanachama wa Taswe (kulia) akitoa maelezo juu ya bidhaa zake na mmoja ya mteja aliyetembelea maonyesho hayo
 Wafanyabiashara kutoka zanzibar wakionyesha bidhaa mbalimbali za kiasili zinazopatikana katika maonyesho ya kimataifa ya TASWE
 Mjasiliamali kutoka Nairobi Kenya, Bi Jesca Alphonce akionyesha namna ya ktumia moja kati ya bidhaa za urembo kwa wateja waliojitokeza kwenye maonyesho hayo
 Mfanyabiasha na mwanachama wa Taswe bi. Elizabeth akionyesha bidhaaa kwa wateja waliotembelea maonyesho
 Maonyesho haya ya akina mama wanachama wa Taswe yanaendelea ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay ambapo yalifunguliwa jana Machi 25, 2017 na kilele chake kitakuwa 31.03.2017.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa