Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, TUTCA YAENDESHA KONGAMANO LENGO KUPAZA SAUTI JUU YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KATIKA MAENEO YA KAZI.

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, TUTCA YAENDESHA KONGAMANO LENGO KUPAZA SAUTI JUU YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KATIKA MAENEO YA KAZI.

 Mgeni Rasmi katika Kongamano la Siku ya wanawake Duniani katika Kupaza sauti juu ya unyanyasasaji wa kijinsia katika maeneo ya kazi Mh. Magreth Sitta (MB) akitoa hotuba yake na kufungua rasmi mjadala
Mkurugenzi wa Jinsia na Vijana TUCTA Bi.Siham Ahmed akizungumza katika Kongamano hilo na kusema kuwa lengo kubwa ni kupanua wigo wa kuwapigania wanawake kwani ukatili huo upo kuanzia ngazi ya familia.
Mwenyekiti wa wanawake Rehema Ludaga akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali waliofika katika Kongamano hilo
 Katibu Mkuu wa TUCTA Dkt. Msigwa akitoa nasaha zake wakati wa kongamano hilo
 Rais wa TUCTA  Bw. Gratian Mkoba akizungumza na wakina mama pamoja na wadau mbalimbali katika Kongamano hilo.
Mwakilishi wa Asasi ya Global Peace Foundation katika Kongamano hilo Anna Mwalongo akichangia jambo
 Mmoja wa washiriki katika Kongamano hilo akitoa salamu za shukurani kwa Mgeni Rasmi wakati wa Kongamano hilo
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika Kongamano hilo
Picha zote na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa

Story na Dickson Mulashani- Funguka Live Blog
 
Katika maadhimisho ya siku  ya wanawake Duniani, Chama Cha Wafanyakazi  nchini (TUCTA) kimeendesha kongamano na wanawake nchini kupitia uwakilishi wa vyama vyao lenye lengo la kupaza sauti juu ya ukatili wa kijinsia hasa unyanyasaji wa wanawake katika maeneo ya kazi ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mh Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Magreth Sitta.

Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi vikiwemo RAAWU, TUGHE,TALGWU,TASU, CWT ,TEWUTA,DOWUTA, TRAWU, CHODAWU,TUICO na COTWU(T)  lililodhaminiwa na SSRA, shirika la kazi duniani ILO kampuni ya Mo Dewji Foundation pamoja na Global Peace Fodation ambao ndio walioshiriki   kufanikisha kongamano hilo lil0beba kauli mbiu isemayo “Kukomesha na Kuzuia Ukatili na Unyanyasaji Dhidi ya  Wanawake Mahala pa Kazi” likilenga  ikilenga  kutanua wigo wa kuwapigania wanawake kwani vita hii ilielemea zaidi katika ngazi za kijamii na hasa familia.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Rais wa chama cha wafanyakazi TUCTA Ndg.Gratian Mukoba amepongeza jitihada zinazofanywa na wanawake katika maeneo waliopo na kuwasihi washikamane na kudumisha upendo baina yao ili kuujenga ukuta imara dhidi ya manyanyaso dhidi yao na kuwaomba wazingatie suala la afya katika maeneo yao ya kazi . “Bila kuwa na afya bora mapambano haya hayatakuwa na tija, ni muhimu kuhakikisha hata maeneo yetu ya kazi yanakuwa na vyoo vya kutosha na vyenye kukidhi mahitaji ya kijinsia ,haipendezi watu wa jinsia moja kushiriki katika maliwato moja na endapo kuna ” alisema Ndg. Mukoba.
Aidha kongamano hilo limebainisha miongoni mwa manyanyaso wanayopata wanawake katika maeneo ya kazi ni pamoja na kiakili na kimwili kutokana na vitendo kama kutopandishwa vyeo,kunyima ruhusa za kwenda masomoni,kupewa uhamisho usio na tija manyanyaso vya kingono ikiwemo hata wakati wa kuomba ajira.
Alipokaribishwa kufungua rasmi kongamano hilo, Mgeni rasmi Mh.Magreth Sitta alijikita kuwahimiza wanawake kujitoa na kugombea katika nafasi mbalimbali katika nyadhifa tofauti ambazo zipo katika maeneo yao ya kazi na maadam wanakidhi vigezo huku akitumia historia yake ya uongozi kama ushuhuda na hamasa kwao.
Sambamba na hilo amewataka akina mama kupitia vyama vyao kuhakikisha wanaweka mikakati makini ili kuweza kushabihiana na malengo ya serikali na kujiweka katika mfumo wa kuchangia kuijenga Tanzania ya Viwanda huku akigusia kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitaifa
Kongamano hili lilianza kufanyika mnamo miaka ya tisini na huadhimishwa kila mwaka siku moja kabla ya tarehe ya kilele ya siku ya wanawake duniani.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa