Na Mwandishi wetu,
Wito umetolewa kwa vijana kuchangamkiwa fursa za
mafunzo ya ujasilrimali ili kupata mfunzo ya stadi za maisha na za
ujasimriamali ili kupunguza tatizo la ajira hapa nchi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC), Bw. Sosthenes Sambua wakati
akizungumza na waandishi wahabari jiji Dar es Salaam, kuwa vijana
wanahitajika kuchangamkia fursa ya mafunzo hayo ili kupata stadi za
maisha na za ujasiliamali.
“Tunawataka vijana wenye umiri wa miaka 18 hadi
24 waweze kuomba fursa hiyo kwa ajili ya kupata mfunzo haya muhimu,” na
kwa kufanya hivyo ni moja ya njia ya kukabiliana na tataizo la ajira
ambalo linawakumba vijana wengi nchini aliongeza kusema,Bw. Sambua.
Alisema mafunzo haya yameingia hatua ya pili
baada ya awamu ya kwanza kufanyika mwaka 2016, na sasa yanawalenga
vijana wa Manispaa za Mtwara Mikindani, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es
Salam, Mkoa wa Dodoma na Kibaha Mkoani Pwani.
Alifafanua kwamba wanaotaka kujiunga fursa hiyo
wanapaswa kupata taarifa zote toka ofisi zao za Kata au ofisi za Maafisa
Vijana za Manispaa na kujaza fomu maaluimu.
Katika kutoa mafunzo hayo TECC inashirikiana na
Taasisi ya Kuendeleza Vijana Kibiashara ya Marekani (IYF),Shirika la
Kuendeleza Viwanda Vidogo Nchini (SIDO),Chama cha Wafanya Biashara wenye
Viwanda na Wakulima (TCCIA),Mfuko wa Rais wa Kujitegemeza (PTF) na
wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfukoa wa Rais wa
Kujitegemea (PTF),Bi. Haigath Kitala alisema serikali na wadau
mbalimbali wa maendeleo wanahitajika kuendelea kuwajengea uwezo vijana
kujiajiri kupitia fursa za program kama hizo.
“Jukumu la kubwa la mfuko wa Rais katika miradi
ya TECC ya kukuza ujasiriamali kwa vijana ni kutoa mikopo nafuu ya
kibiashara kwa vijana baada ya mafunzo kama haya kutolewa,”
Alisema pia wanafanya ufuatiliaji na kufanya
tathimini ya mpango mzima wa mikopo ya mfuko wa Rais na manufaa yake kwa
walengwa, na kuhakikikisha kuwa mikopo inarudishwa.
Meneja Biashara wa Chama cha Wafanya Biashara
wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA),Bi.Zahra Mahmoud alisema jukumu la
katika program hiyo ni kukuza ujasiriamali kwa vijana ni kutambua na
kupendekeza wafayanyabiashara kusaidia vijana mawazo na mwongozo sahihii
kwa njia ya malezi ya kibiashara.
“Hili ni jukumu ambalo ni letu na
hatuwezi kulikwepa na tunataka nchi yetu iwe wajasirimali wengi, kukuza
ajira na uchumi,”alisisitiza.Bi. Mahmoud.
Naye Afisa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.
Masalida Njashi aliwataka vijana wa mkoa wa Dar es Salaam kuitikia wito
huo ili kuweza kuwa na mafunzo yatakayowawezesha kujimudu kimaisha.
Program ya Via Jiandalie Ajira inafadhiliwa na The MasterCard Foundation.
0 comments:
Post a Comment