Na Husna Saidi & Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Serikali
ya Jamhuri ya Afrika Kusini imekubali kuendelea kuwafudisha marubani wa
Tanzania ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukuza maendeleo ya sekta ya
uchukuzi na usafiri wa anga pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya
nchi hizo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga
ameyabainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi
kuhusu majadiliano ya awali yaliyofanyika kati ya nchi hizo mbili juu
ya mikataba mbalimbali inayotegemewa kusainiwa Mei 11 mwaka huu.
Balozi
Mahiga alisema kuwa katika majadiliano hayo wamejadili mikataba
iliyowahi kusainiwa kwa kupima utekelezaji wake pamoja na kujadili
mikataba mipya iliyojikita katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo
za uchukuzi, nishati, elimu pamoja na mawasiliano.
“Katika
sekta ya uchukuzi tumekubaliana kuboresha barabara, usafiri wa anga
pamoja na reli hasa ya TAZARA, sisi tumenunua ndege na tunaendelea
kununua zingine zitakazosafiri hadi Afrika ya Kusini hivyo nchi hiyo
imekubali kuendelea kuwafundisha marubani wa Tanzania kuendesha na
kukarabati ndege hizo,”alisema Balozi Mahiga.
Aliongeza
kuwa mikataba hiyo inayotarajiwa kusainiwa hapo kesho imelenga maeneo
ambayo yatapewa kipaumbele katika ushirikiano huo yakiwemo ya uchumi,
biashara na uwekezaji pia mikataba hiyo imewekewa utaratibu wa
ufatiliaji na utekelezaji wake.
Akiongea
kuhusu kulinda uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana - Mashabane
alisema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kutafsiri ushirikiano
wa kihistoria uliopo baina yetu na kuufikisha kwa kizazi hiki na
kijacho kwani kwa kusoma tu historia katika vitabu ni rahisi kwao
kusahau hivyo mkutano huo utapelekea kuendeleza na kurithisha uhusiano
uliopo baina ya vijana wa nchi hizo mbili.
“Tanzania
na Afrika Kusini tuna historia kubwa ya kushirikiana katika harakati za
kutafuta ukombozi wa nchi zetu lakini haitoshi kuwa na urafiki wa
kihistoria tu bali tuwe na urafiki utakaoleta maendeleo katika nchi
zetu”, alisema Bi. Maite.
Nae
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kuwa
nchi ya Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi nne zinazowekeza nchini
kwa kiasi kikubwa hivyo tayari wana mikataba mbalimbali ambayo
wanaendelea kuiboresha ili kuendelea kukuza uchumi kupitia sekta ya
viwanda.
“Tumeshaongea
na Waziri mwenye dhamana ya viwanda wa Afrika Kusini kwamba kuna ardhi
kubwa katika eneo la Kilombero 1 na Kilombero 2 hivyo waongeze nguvu ya
kuwekeza katika uzalishaji wa sukari kwenye eneo hilo,”alisema Mwijage.
0 comments:
Post a Comment