Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UMASKINI WATAJWA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU

UMASKINI WATAJWA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 




Na Mwandishi Wetu.
Hali ngumu ya maisha ikiwepo ukosefu wa mahitaji muhimu imetajwa kama sababu kubwa inayochochea Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu huku waaathirika wa biashara hiyo wakiahidiwa maisha mazuri katika nchi wanazopelekwa.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa  Binadamu (ATP), ambaye pia ni mgeni rasmi katika mafunzo hayo, Adatus Magere amesema  wahusika wa biashara hiyo wamekua wakiwarubuni waathirika wa biashara hiyo kuwapatia  maisha mazuri na kujikuta wakiingia katika madhara ya biashara hiyo.
Aliongeza kuwa   kuna umuhimu kwa watunga sheria na vyombo vya sheria kutunga sheria zitakazo saidia kutokomeza kabisa biashara hiyo kwani imekua ikiendelea kukua siku hadi siku hali inayopelekea idadi ya wahanga wa biashara hiyo kuendelea kuongezeka.
“Tunaomba watunga sheria na wasimamiaji wa sheria kusaidiana kwa pamoja katika kudhibiti na kuzuia biashara hiyo kwa kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuhusika moja kwa moja na biashara hiyo ili tatizo hili liweze kuisha katika nchi zetu,” alisema Magere.
Aidha Katibu Mkuu wa Sekritarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu ambaye pia ni mwenyeji kwenye mafunzo hayo, Seperatusi Fella, amesema kuwa ili kuweza kupambana na kuzuia biashara hiyo kuna umuhimu kwa wadau mbaimbali kutoa elimu na mafunzo juu ya athari zitokanazo na usafirishaji haramu wa binadamu, hivyo mafunzo ya mara kwa mara ni muhimu kwa wananchi na wadau mbalimbali.
Naye Mratibu wa mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa (IOM), Tamara Keating  ameahidi kushirikiana na mashirika mbalimbali ili kukomesha biashara hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ili kupata  taarifa ya wahusika wa biashara hiyo.
Ripoti na tafiti mbalimbali za kimataifa juu ya biashara hiyo zinaonesha Tanzania ni mojawapo kati ya nchi nyingi zinazohuishwa na biashara haramu ya usafirishaji binaadamu ambapo waathirika wengi wa biashara hii ni watoto walio chini ya umri wa  miaka 18 na kuendelea wanaoahidiwa kazi nzuri na maisha mazuri pindi wafikapo katika nchi wanazopelekwa.
 Mafunzo hayo yanafanyika  katika  hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuleta uelewa wa jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa pamoja na kuleta ushirikiano katika kukomesha biashara haramu ya usafirishaji binadamu baina ya wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.




 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa