Kuelekea siku ya kuchangia damu duniani,
Hospitali ya Sanitas iliyopo Mikocheni, iliandaa Kambi ya kuchangia Damu
Leo Jumanne, Tarehe 13 Juni 2017.
Katika Kambi hiyo zaidi ya chupa 50 za damu zilikusanywa na Damu Salama.
Waliochangia Damu ni watu kutoka nje Pamoja na Staff wa Sanitas Hospital.
Kwa kuchangia chupa moja ya damu, unaweza kusaidia Watanzania watatu.
Damu inahitajika mahospitalini kwa kuokoa maisha ya Kundi yafuatayo:
- wajawazito waliokuwa na tatizo wakati wa kujifungua
- watoto waliokuwa na upungufu wa damu
- watu waliokuwa na ugonjwa wa sikla
- watu waliokuwa wamepata ajali na wanaofanyiwa upasuaji
"Kuna Uhaba wa Damu, Hakikisha unaonyesha
uzaleno na upendo wako kwa Watanzania wenzio kwa kuchangia damu na
kuokoa maisha yao" - Alisema Dr. Sajjad Fazel, meneja msaidizi wa
Hospitali ya Sanitas
0 comments:
Post a Comment