Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Serikali Yaanzisha Rejesta ya Wanaohisiwa Kuwa na Kifua Kikuu.

Serikali Yaanzisha Rejesta ya Wanaohisiwa Kuwa na Kifua Kikuu.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na: Lilian Lundo - MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanzisha rejesta ya wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu itakayowekwa  katika kila ngazi ya utoaji wa huduma za Afya hapa nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo, leo Mjini Dodoma, katika mkutano wa kupitia utekelezaji wa mkakati wa uboreshaji wa kasi ya uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu nchini.
Ummy amesema Serikali inayo wajibu wa kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa, ili kufikia lengo hilo.
Kutokana nna dhamira hiyo njema Wizara kwa mara ya kwanza imeanzisha rejesta mpya ya wanaohisiwa kuwa na kifua kikuu itakayowekwa katika kila ngazi ya utoaji wa huduma za Afya hapa nchini.
“Tayari rejesta hizi zimesambazwa na kuanza kutumika katika mikoa 16 iliyoanza kutekeleza zoezi hili,” amesema Ummy.
Waziri Ummy aliongeza kuwa mkakati wa uboreshaji kasi ya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ni mkakati uliojaa mbinu za kiuendeshaji ili kuvipa uwezo vituo vya huduma za Afya kufanya uchunguzi wa kina kwa kila mteja anayepata huduma vituoni na kuwapata wote wenye kuugua kifua kikuu na kuwaanzishia matibabu.
Ummy amesema mkakati huo unahusisha zana zinazotoa mwanga na kuangaza njia bora za kuchunguza kifua kikuu na kubaini wote wenye kuugua katika jamii mijini na vijijini.
Vile vile amesema, mkakati huo umejaa mbinu za kiuendeshaji ili kuvipa uwezo vituo vya huduma ya Afya kufanya uchunguzi wa kina kwa kila mteja anayepata huduma vituoni na kuwapata wote wenye kuugua kifua kikuu pamoja na kuwaanzishia matibabu.
Pia utatoa fursa kwa kila kitengo kujitathmini ili kuweka misingi timilifu ya uchunguzi wa kifua kikuu kwa wateja wote wanaohudhuria matibabu katika eneo husika.
Aidha, amesema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ulianza mnamo Julai, 2016, ambapo ni mwaka mmoja sasa tokea vituo vya mwanzo katika Mikoa ya Mbeya na Dodoma ianze kuweka msukumo mpya. Kuanzia hapo, Mikoa 16, wilaya 48 na vituo 187 nchini kote vimeweza kuanza utekelezaji.
Masuala ya ubora wa huduma za afya yamepewa kipaumbele katika mkakati mpya uliotolewa na Shirika la Afya Duniani wa kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2035.



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa