Na: Paschal Dotto Na Thobias Robert -MAELEZO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amezindua rasmi mfumo wa huduma ya kutuma pesa kwa njia ya simu za
mkononi wa kampuni ya mawasiliano ya TTCL ujulikanao kama “TTCL PESA”
katika Makao Makuu ya Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
Akizindua
mfumo huo Jijini Dar es Salaam leo, Makamu wa Rais amesema kuwa, TTCL
imetekeleza agizo la serikali ya awamu ya tano lililoyataka mashirika
yote ya Umma yajiendeshe yenyewe kwa faida, pia kuwahudumia wananchi na
kuondoa urasimu ambao umekuwa ukifanywa na Makampuni ya kigeni.
“Kuzinduliwa
kwa huduma hii ni udhibitisho mwingine kwamba TTCL kama kampuni
inayomilikiwa na serikali imejidhatiti kutekeleza kwa vitendo azma ya
Dkt Johm Pombe Magufuli inayotaka Mashirika yote ya Umma kujiendesha kwa
faida na kutoa gawio kwa serikali’’ . Alisema Makamu wa rais.
Kampuni
ya TTCL inaimarika kiutendaji ili kuendana na mabadiliko ya kidijitali,
kwa kudhihirisha hilo waliweza kuibuka washindi wa kwanza katika
maonesho ya 41 ya Kimataifa ya kibiashara ya Sabasaba katika utoaji wa
huduma ya mawasiliano nchini Tanzania.
Kuanzishwaa kwa huduma
kutafungua fursa za kibiashara na utoaji wa huduma kwa watu mbalimbali
yakiwemo maeneo ya vijijini, kama kutuma na kupokea pesa, kulipia
huduma mbalimbali kama vile bili za umeme na Maji, pia koungeza pato la
taifa kupitia kodi ya miamala itakayokuwa inafanywa.
Mafanikio
ya Kampuni hiyo yamechagizwa na uamuzi wa serikali wa kuirudisha
mikononi mwake na kuiundia bodi mpya na menejimenti ambayo jukumu lake
kubwa ni kuiendesha kiushindani na kibiashara ili kuendana na mabadiliko
ya soko.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi
ya TTCL Bw. Omary Nundu amesema kuwa, Kampuni hiyo ina mpango wa
kuanzisha utengenezaji wa simu hapa nchini, lakini pia ametoa wito kwa
wananchi kuanza kutumia huduma ya TTCL kwani ni kampuni ya serikali
hivyo watadhihirisha uzalendo kwa nchi yao pamoja na kuikuza Kampuni
hiyo kimapato.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Maria Sasabo amesema
kuwa serikali inazidi kuimarisha Kampuni hiyo ili iweze kuingia katika
soko la ushindani wa mawasiliamno na makapmuni menginhe yanayotoa huduma
hizo, kama vile, Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel, Smart pamoja na
Zantel.
TTCL ni kampuni pekee nchini yenye mtandao mkubwa wa
mawasiliano unaotumika katika ofisi za serikali na baadhi ya Taasisi
binafsi, kwa kuzingatia kuwa wao ndio wamiliki wa mkongo wa taifa wa
mawasiliano ambao umeleta mabadiliko makubwa katika Nyanja ya
mawasiliano hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment