Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda
(katikati) akifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Mwezeshaji, Dkt
Donath Olomi hayupo pichani wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa
ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza
ujasiriamali hapa nchini, wapili kushoto Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa, kushoto ni
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na
Maendeleo ya Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini, wa pili kuli ni
Mkurugenzi Msaidizi Mazingira ya Biashara Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.
Christopher Mramba na kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa baraza hilo,
Bi. Anna Dominick.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda
(katikati) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa, wakati wa mkutano
wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa
kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, na kulia ni Mwakilishi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya
Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini.
Wadau
kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika makundi wakati wa mkutano
uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa
wa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, aliyesimama ni mwezeshaji wa
mkutano huo, Dkt. Donath Olomi.
Watanzania
wametakiwa kutumia fursa zinazoendelea kuwekwa na serikali ya awamu ya
tano kujikita katika ujasiriamali na kuanzisha viwanda kwa ajili ya
kujenga uchumi viwanda ili kufikia uchumi kati na kuboresha ustawi wa
jamii hapa nchini
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda
alisema hayo wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya
mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa
nchini, kuwa wakati wa watanzania kujikita katika ujasiriamali na
kuwekeza katika viwanda umewadia.
“Wakati
wa watanzania kuanzisha viwanda kuzalisha bidhaa zinazotokana na mali
ghafi za hapa nchini umewadia,” na hakuna wakati mzuri zaidi kuliko
kipindi hiki ambacho serikali imweka kipaumbele zaidi katika hili,
aliongeza kusema Profesa Mkenda.
Mkakati
huo wa kitaifa wa kuendeleza ujasiriamali umeandaliwa na Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na
Maendeleo ya Biashara (UNCTAD).
Profesa
Mkenda alifafanua kwamba serikali imeamua kuja na rasimu hiyo kupata
mkakati wa uendelezaji ujasiriamali huku ikitambua uchumi wa Tanzania
utajengwa na watanzania na wawekezaji wa nje kuja kuongezea tu.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi.
Beng’I Issa alisema Baraza lake linasimamia sera ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi na suala la uasiriamali ni nguzo muhimu katika uwezeshaji
wananchi.
“Pendekezo
la mkakati huu wa kuendeleza ujasirimali umeandaliwa kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali na leo ni siku ya pekee kwa wataalaam kutoa maoni
yenu ili kupata mkakati wa kitaifa,” na aliwaomba watalaamu hao kutoa
maoni yao kukamilisha upatakanaji wake, alisema, Bi. Issa
Alisema jukumu la kuaandaa mkakati wa kitaifa wa kuongoza ujasiriamali
kufikia uchumi wa kati na wa viwanda ni muhimu kwa vile utawezesha
kupata wajasiriamali wenye mafanikio walioongozwa vyema.
Alisema
uandaaji wa rasimu hiyo umeangalia mapungufu yaliyopo katika nchi na
umekuja na majibu ambayo ni rafiki kwa wajasiriamali.
Alisema
hadi kufikia Agosti mwezi ujao maoni yote ya wadau yatakuwa yameingizwa
na matarajio yaliyopo ni kwamba mkakati huo utaweza kuwa tayari Octoba
2017 kwa ajili ya kuendeleza ujasiriamali.
Mwakilishi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya
Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini alisema shirika hilo limeweka suala
la uendelezaji ujasirimali katika ajenda kuu na Tanzania inapofanya
hivyo inaendana na ajenda hiyo.
“Katika
kukuza ujasiriamali kuna changamoto mbalimbali ambazo nchi nyingi za
Afrika zinakabiliana nazo na kuwepo kwa mkakati huo nchini Tanzania
itasaidia katika hili,” na kuongeza mkakati huo pia usaidie kuja na sera
inayoleta usawa kwa wajasiriamali.
Alisema
vikwazo vikuu katika mataifa haya katika ujasiriamali na biashara ni
pamoja na vikwazo vya kisheria, upatakanaji wa mitaji kutoka taasisi za
kiedha, na uhafifu wa teknolojia na mawasiliano .
0 comments:
Post a Comment