Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UCHIMBAJI NA UCHOTAJI MCHANGA KIHOLELA WASITISHWA

UCHIMBAJI NA UCHOTAJI MCHANGA KIHOLELA WASITISHWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NA; EVELYN MKOKOI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina ,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.
Pia ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.
Akitoa agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba mchanga.
Alisema ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.
“Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza Mpina
Alisema watafanya Operasheni ya usiku na mchana kuhakikisha watu watakaoendelea kuchimba mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa