Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda akizungumza
katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam leo wakati
wakisheherekea miaka 20 ya benki ya Exim Tanzania pamoja na kutoa msaada
wa Vitanda na Magodoro 40 katika hospitali hiyo ikiwa benki hiyo
inaijali jamii. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Matawi ya Exim Tanzania, Agnes
Kaganda, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim
Tanzania, Stanley Kafu. Na kutoka Kulia ni Katibu wa Afya, Sanura Kondo
na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi(Katikati) akiwashukuru
Benki ya Exim mara baada ya kutoa msaada wa Magodoro na Vitanda 40
katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda na Kulia ni Katibu wa Afya, Sanura Kondo na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi.
BENKI
ya Exim
Tanzania imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 katika hospitali ya
Wilaya ya Temeke ikiwa ni shukrani yao katika kuadhimisha miaka 20 ya
Benki hiyo ya kujali jamii ambapo msaada huo utawekeza shilingi milioni
200
katika sekta ya afya Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda wakati wa
kuwakabidhi vitanda 40 katika hospitali ya wilaya ya Temke jijini Dar es
Salaam leo. amesema kuwa
Mradi huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda
katika hospitali nchini hivyo benki ya Exim itatoa magodoro 500 na vitanda katika
hospitali za serikali mikoa 13 nchini.
“ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea
miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim
imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini.
Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi
tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo
mbalimbali nchini.” amesema Ponda
Ikiwa
kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya
Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali, katika mikoa
ya Mbeya, Iringa, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga,
Mtwara, Pemba na Unguja.
0 comments:
Post a Comment