Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KAMPENI YA HAKI YA ARDHI KWA WANAWAKE ITAKAYOENDESHWA NA OXFAM NA TALA KUWASAIDIA WANAWAKE KUMILIKI ARDHI.

KAMPENI YA HAKI YA ARDHI KWA WANAWAKE ITAKAYOENDESHWA NA OXFAM NA TALA KUWASAIDIA WANAWAKE KUMILIKI ARDHI.

Muwezeshaji Bw. Evans Rubara akiendelea kutoa mwongozo wakati wa mkutano wa wadau kuhusu maswala ya Ardhi ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania wakishirikiana na TALA kujadili namna gani watakavyoweza endesha kampeni ya kuwawezesha wanawake kumiliki Ardhi
Mratibu wa Kampeni ya Ardhi Kutoka Oxfam Bi. Naomi Shadrack(wa katikati) akitoa maelekezo namna gani walivyojipanga katika kutekeleza kampeni hiyo ya kumuwezesha mwanamke kumiliki Ardhi
Bi. Eluka Kibona Mkuu wa kitengo cha ushawishi na utetezi kutoka Shirikika la kimataifa la Oxfam Tanzania akichangia maswala mbali mbali na kusema  kuwa mfumo dume unachangia kwa kiasi kikubwa kwa wanawake kuto kumiliki ardhi licha ya kwamba wao ndio ambao kwa kiasi kikubwa wanasaidia katika kuzalisha mazao ya chakula, na kuongeza kwamba kupitia  kampeni hiyo wanawake wengi watapata uelewa  na kuwasidia kumiliki Ardhi.
Mmoja wa wachangiaji Bw. George Rodgers akichangia jambo wakati wa mkutano huo
Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Care International Bi. Mary Ndaro akitoa ushauri namnagani wataweza kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na wanawake wengi zaidi wanapata uelewa wa namna wanavyoweza kumiliki ardhi.
Mmoja wa wadau akichangia jambo na kushauri kuwa ni muhimu kuwashirikisha hata wabunge wakati wa kampeni hiyo.
Mshauri wa mambo ya Jinsia kutoka shirika la kimataifa la utafiti wa mifugo Bi. Josephine Dungumaro akielezea ni namna gani ambavyo wadau mbalimbali watashirikishwa ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Mkutano ukiwa unaendelea 
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa 

Shirika la kimataifa la Oxfam Tanzania wakishirikiana na TALA wanatarajia kuendesha kampeni ya itakayolenga kumwezesha mwanamke kuelewa haki yake na maswala mbali mbali katika kumiliki Ardhi.
Hayo yamesemwa katika mkutano wa wadau wa kutetea haki na asasi za kiraia nchini mkutano ulioandaliwa na Shirika la kimataifa la Oxfam Tanzania wakishirikiana na Jukwaa la Ardhi ( TALA).

Akizungumza wakati wamkutano huo  Eluka Kibona Mkuu wa kitengo cha ushawishi na utetezi kutoka Oxfam alisema kuwa mfumo dume ni moja ya changamoto ambazo zinakwamisha kwa kiasi kikubwa kwa wanawake kupata haki ya kumililisha ardhi, na kuongeza kuwa kupitia kampeni hiyo wanawake wengi watapata uelewa na kupata nafasi na wao kumiliki ardhi.

Nae Mratibu mkuu a kampeni hiyo Naomi Shadrack alisema kuwa lengo kubwa la kampeni hiyo ni kuleta ukombozi kwa mwanamke na kumpatia Elimu itakayomuwezesha kutambua thamani ya ardhi ambayo atakuwa anaimiliki, aliongezea kuwa wanawake wengi wanatumia ardhi kwa ajili ya kilimo hasa kuzalisha mazao ya chakula na wanauwezo wa kuwa na umiliki wa ardhi hiyo.

Wadau wengine walioshiriki katika mkutano huo ni Care International,WLAC,PINGOs,UCRT,FFH,LANDESA,PWC,NES,ILRI

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa