Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MASHINE YA KUCHAKATA MKAA KUSAIDIA KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

MASHINE YA KUCHAKATA MKAA KUSAIDIA KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


 Na. Paschal Dotto

Serikali ya Awamu ya Tano inaonyesha dhamira ya dhati ya kujenga Taifa lenye uchumi wa viwanda. Ujenzi wa viwanda utapunguza ama kuondoa changamoto ya ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. 

Fursa za uwekezaji katika viwanda ni jambo ambalo Mhe. Rais John Pombe Magufuli amekuwa akilisisitiza katika hotuba zake. Kwa kuzingatia hilo, wajasiriamali na wawekezaji wameaanza kujitokeza katika ujenzi na ufufuaji wa viwanda.

 Katika makala hii utamwona mtanzania ambaye amebuniu teknolojia ya kutengeneza mkaa bila kuathiri mazingira. 

 Mjasiramali huyo ambaye ametumia fursa hiyo ni Bwana Leonard Gabriel Kushoka ambaye ameanzisha kampuni ya kutengeneza na kuchakata nishati ya mkaa kwa kutumia mashine maalumu katika kampuni yake ya Kuja na Kushoka Tools Manufactured Group ambayo makao yake yako Tabora.

 Hii ni teknolojia ya pekee ambayo utapata nishati ya mkaa bila kuathiri mazingira pia inatoa mwelekeo mzuri katika kuelekea uchumi wa taifa la viwanda ambayo ni sera ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. Magufuli , katika kutambua mchango wa wadau mbalimbali Serikali inaunga mkono kwa yeyote mwenye fikra pana juu ya teknolojia yeyote anapaswa kutoa wazo. 

 Kushoka amesema katika upande wa mazingira kitu kikubwa kinachohitajika ni kuyatunza kwa kuyaweka katika hali nzuri lakini pia kwa kupanda miti na kuitumia ipasavyo katika kupata hewa safi.

 Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Da es Salaam tarehe 12 Julai 2017 Kushoka alikuja na mashine ambayo kwa hakika ni mashine ya kujivunia kwa Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda.

 Katika mkutano huu mashine hiyo ambayo kwa lugha ya kigeni inaitwa “Charcoal Ubiquity” ambayo ina uhakika wa kuzalisha mkaa bila kuathiri mazingira ya binadamu na watumiaji wa nishati hii muhimu ilitolewa ufafanuzi.

 Kwa mujibu wa takwimu za Wakala wa Misitu (TFS) Dar es Salaam inatumia magunia 28000 ya nishati hiyo ambayo ni sawa na tani 1600 kwa siku ambayo ni sawa na asilimia 50 kwa nchi nzima huku majiji ya Mwanza na Arusha wakifuatia katika takwimu hizo.

Kushoka anasema pia katika kupata nishati hiyo kienyeji inatumia tani 12 za miti kwa tani 1 moja ya mkaa kwa hiyo kwa takwimu hizo za Dar es Salaam zinaonyesha ni jinsi gani uharibifu wa mazingira unatokea katika misitu asili ya nchi yetu. Katika matumizi sahihi ya teknolojia hii ya Kushoka Tools Manufactured Group ni kujivunia kwa nchi yetu kuelekea kutimiza sera ya awamu ya tano inayoelekea kuijenga Tanzania ya viwanda , mashine hii yenye kutumia takataka za aina yeyote ikiwemo mabaki ya mazao isipokuwa plastiki katika kuzalisha mkaa kwa matumizi ya nyumbani Katika teknolojia yake Bwana Kushoka alisema mashine hii ina uwezo wa kuzalisha wastani kilo 160 kwa saa moja , pia inahitaji watu 7 katika ufanyaji kazi wake ambao wanahitajika kwa kuiwezesha katika kuchakata nishati hiyo ya mkaa, na ina uwezo wa kutoa magunia 20 kwa siku jambo ambalo linarahisisha maisha na matumizi ya nishati hiyo majumbani. 

 Katika ufumbuzi huu ambao pia utakuwa bora kwa kutoa ajira kwa vijana kwani katika viwanda vidogo vidogo vitakvyoanzishwa vitakuwa na watumishi na kusaidia kuondoa kero ya ajira kwa vijana Bwana Kushoka anasema kuwa malighafi zinazotumika katika mashine hiyo ni takataka za aina yoyote isipokuwa vitu vya plastiki, kwa hiyo kwa watumiaji wa mashine hii wanapaswa kujua kuwa plastiki siyo malighafi ya mashine hii. 

Kwa takwimu za mazingira jiji la Dar es Salaam linazalisha tani 5000 kwa siku kwa hiyo ni vyema teknolojia hii ikatolewa kwa elimu kubwa ili kusaidia utunzaji wa mazingira. 

Katika matumizi ya mashine hii ni kitu ambacho ni muhimu zaidi katika kutumia teknoljia hii, zaidi mashine hii ya kujivunia kwa nchini yetu inatumia nishati ya mafuta ya diseli na umeme lakini sanasana inategemea na maamuzi ya mtumiaji au mnunuzi wa mashine hii, ila kwa wale walioko vijijini ambako hasa nishati ya umeme haipatikani kirahisi wanashauriwa kupata mashine itumiayo diseli ili kuepusha usumbufu wa matumizi ya teknolojia hii. 

 Akizungumzia mabaki ya mazao kutoka mikoa ambayo huzalisha mazao mbalimbali ikiwemo tumbaku, karanga, mpunga, mahindi, Kushoka alitaja baadhi ya mikoa hiyo kuwa ni Tabora, Shinyanga, Mwanza na Rukwa.

Maeneo hayo yanapswa kupata teknolojia hiyo ikizingatiwa malighafi inapatikana kiurahisi na kutumika katika kuchakata mkaa hatua ambayo inasaidia kutunza uoto wa asili nchini. Katika matumizi ya mashine hii ni kitu ambacho ni muhimu zaidi katika kutumia teknoljia hii, zaidi mashine hii ya kujivunia kwa nchini yetu inatumia nishati ya mafuta ya diseli na umeme lakini sanasana inategemea na maamuzi ya mtumiaji au mnunuzi wa mashine hii, ila kwa wale walioko vijijini ambako hasa nishati ya umeme haipatikani kirahisi wanashauriwa kupata mashine itumiayo diseli ili kuepusha usumbufu wa matumizi ya teknolojia hii.

Kwa Dar nes Salaam tayari kuna vituo vinne ambayo elimu kuhusu teknolojia hii ishatolewa vituo kama Pugu, Tandika, Tegete pamoja na Mbezi Kimara kwa hiyo kwa wakazi wa jiji la dar es salaam wanatakiwa kutembelea vituo hivyo kwa elimu na kupata mashine hiyo yenye teknoljia ya kisasa Kwa watanzania wote tunatakiwa kuunga mkono jitihada hizi kubwa zinazo fanywa na kuja na kushoka tools manufactures group, kwa kununua mashine kwa matumizi kuchakata mkaa na kutunza mazingira kwa usafi wa nchi yetu kwa maendeleo ya taifa, kupata mashine hii ya kujivunia katka mapinduzi ya viwanda inategemea na mahitaji ya mnunuzi kwani mashine hii inauzwa kuanzia shilingi milioni 3 mpaka milioni 15 kutokana na maamuzi lakini bila kusahau matumizi ya mtumiaji katika teknolojia hii ya kisasa.

Taifa letu, serikali ni yetu, mistu ni yetu tunatakiwa kutumia mazingira vizuri kwa kupanda na kutunza mistu yetu ,nunua mashine ya kuchakata mkaa ili kuepusha ukataji miti ovyo na kuharibu mazingira.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa