Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SERIKALI YAITENGEZEA NIT SH6.7 BIL

SERIKALI YAITENGEZEA NIT SH6.7 BIL

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Serikali imekitengeza Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) bajeti ya Sh6.7 bilioni ambazo zimeanza kutmika kuboresha miundombinu kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha utendaji wake.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Jumapili, Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa alitaja baadhi ya miundombinu ambayo imeboreshwa kuwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, ofisi za walimu pamoja na kununua vifaa vya kufundishia.
Profesa Mganilwa alisema kwa sehemu kubwa vyumba vya madarasa vimeboreshwa na kwamba chuo kinakusudia kuweka mkazo kwenye vifaa vya kufundishia katika sekta za anga na reli ili kwenda na wakati.
“Tangu kuanzishwa kwa chuo serikali haijawahi kutenga pesa nyingi kama zilizotengwa mwaka huu, fedha hizo zitakiboresha chuo kwa kutoa wataalamu wa kisasa wakiwemo wa mambo ya usafiri wa reli, tutahama kutoka teknolojia ya treni za zamani au locomotive na kuwa na wataalam wa reli ya kisasa ambayo serikali imeanza kujenga,” alisema Profesa Mganilwa.
Alisema Chuo hicho ni cha kipekee kinachotoa wataalam wa aina yake katika ukanda huu wa Afrika na kwamba kinadahili wanafunzi waliofaulu kidato cha nne kwa masomo ya cheti na diploma na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kwa masomo ya shahada.
“Chuo kinatoa mafunzo katika mfumo unaotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi yaani Nacte na mfumo unaozingatia elimu kwa vitendo yaani CBET ambao unampa uwezo mkubwa mwanafunzi kufanya kushindana katika soko la ajira,” alisema.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa majini na nchikavu (Sumatra), Giliard Ngewe, alisema Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ni muhimili wa uchumi na kwamba bila usafirishaji ushumi hauwezi kukua.
“Chuo hiki kina mchango mkubwa sana kwa taifa, wapo watalaamu wengi wanaosimamia uchumi wa taifa sasa nikiwemo mimi mwenyewe tumesoma hapa na wanasimamia sekta mbalimbali na wengine ni wakurugenzi wa wizara wote ni matunda ya chuo hiki,” alisema Ngewe.

Chanzo Mwananchi


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa