Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UKATILI WAPAA, WATU 479 WAUAWA

UKATILI WAPAA, WATU 479 WAUAWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Imeandikwa na Lucy Lyatuu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba
WATU 479 wameuawa nchini kutokana na vitendo vya ukatili ukiwamo wa watu kujichukulia sheria mkononi katika kipindi cha nusu mwaka 2017, ikiwa ni mara tatu ikilinganishwa na mwaka uliopita, jambo linaloonesha kuwapo ukiukwaji wa haki.
Aidha katika matukio hayo, Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa watu kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa na matukio 117 yaliripotiwa polisi, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya wenye matukio 33, Mara (28) na Geita (26). Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ripoti ya hali ya haki za binadamu kwa kipindi cha nusu ya Mwaka 2017.
Ripoti hiyo inaonesha hali za binadamu kuwa bado ni mbaya kwa kipindi cha nusu mwaka ikilinganishwa na miaka iliyopita. Dk Bisimba alisema ripoti hiyo inayoanzia Januari hadi Juni mwaka huu inaonesha kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kiraia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake na watoto.
Kuhusu kujichukulia sheria mkononi, alisema taarifa za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa matukio ya mauaji kwa watu kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakipungua kwa kati mwaka 2013 mpaka 2016 kutoka vifo 597 mpaka vifo 135. “Hata hivyo, matukio hayo imeonekana kujirudia tena kwa kasi ambapo na kufikia mara tatu ya idadi ya mwaka jana,” alisema Bisimba.
Alisema Jeshi la Polisi linapaswa kushughulikia haraka tatizo la kuwapo matukio hayo na kuhakikisha watuhumiwa wa matukio hayo wanafikishwa mbele ya sheria. Aidha, Bisimba alisema Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kwa pamoja yanatakiwa kuhakikisha kuwa askari wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya raia wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Kuhusu haki za wanawake na watoto alisema matukio ya ukiukwaji wa haki za makundi hayo yameendelea kuripotiwa kwa kiwango kikubwa nchini na taarifa ya Jeshila Polisi kwa kipindi cha Januari hadi Machi, inaonesha kumekuwa na matukio 2,059 ya ubakaji yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali. Mtafiti wa LHRC, Fundikila Wazambi alisema ripoti hiyo inatokana nautafiti mbalimbali uliofanywa na kituo hicho wenye lengo la kuangalia ukiukwaji wa haki za binadamu.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa