Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » VIWANDA 42 ZAIDI KUUNGANISHWA MFUMO WA GESI

VIWANDA 42 ZAIDI KUUNGANISHWA MFUMO WA GESI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani


Na Said Ameir-MAELEZO

Serikali imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa haraka.

“Tuna gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza Waziri Kalemani.Kwa hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki. 

Waziri Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Katika maelezo yake kwa kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea gesi asilia huko Kinyerezi na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi hiyo ya Kinyerezi I na Kinyerezi II, Naibu Waziri huyo alidokeza kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia ili iweze kusafirishwa nchi za nje.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC kutayarisha mpango maalum kwa kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo yatawekewa miundombinu ya gesi ili uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa