Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NAIBU KATIBU MKUU, NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI

NAIBU KATIBU MKUU, NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kushoto) katika kikao chake kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2017. Kikao hicho kilishirikisha wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA), Chalers Sangweni (kulia) na mjiolojia kutoka mamlaka mamlaka hiyo, Simon Nkenyeli (kushoto) wakifuatilia majadiliano mbalimbali katika kikao hicho.
Mtaalam wa Masuala ya Nishati kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini, Jorgen Eriksson (kushoto) akieleza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt ( wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao hicho.  

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa