Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Utaratibu wa utoaji wa matibabu ya Saratani bure kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile akifatilia kwa makini
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile wakipokea vifaa ivyo vilivyotolewa kwa lengo la kufanya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti kwa wanawake nchini ambapo vifaa ivyo vitasambazwa katika vituo vya afya mbalimbali vitakavyotoa huduma hizo
Na Globu ya Jamii, Dar es Salaam
Wanawake
wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kupima saratani ya shingo ya
kizazi pamoja na matiti ili kusaidia kupunguza ongezeko la ugonjwa huo
na kutakiwa kuwahi mapema kupima kabla ya tatizo kuwa kubwa kwani
saratani inaweza kutibika kwa gharama nafuu kabisa.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na
watoto Ummy Mwalimu na kusema kuwa vituo vya afya vihakikishe vinatenga
siku maalum kila mwezi kwa lengo la wanawake kupatiwa huduma ya upimaji
wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi na huduma hizi
zinatolewa bila malipo ili kuhamasisha upimaji kwa wanawake hapa nchini.
"Wanawake
wajitokeze kwa wingi katika kupima ili kujua afya zao na hii itasaidia
kupunguza saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi kwa kina
mama,kuliko kusubiri tatizo liwe kubwa kwani tatizo likiwa dogo saratani
inatibika na kwa gharama ndogo kabisa kuliko kukaa na kusubiri kuwa
kubwa ". Amesema
Amesema
katika kuboresha huduma hizo serikali imenunua mashine za kisasa kabisa
100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa
ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi
173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.
Aidha
Waziri ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji wanaowarubuni watu kuwa
wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kutokana na miti shamba na kuwataka
kuachana na hio tabia Mara moja kwani dawa za asili hazitibu saratani
ila zinatuliza tu.
"
Hakuna dawa ya tiba asili inayotibu saratani waganga wa kienyeji waache
tabia ya kuwarubuni wananchi kuwa dawa hizo zinatibu saratani jambo
ambalo siyo kweli ila dawa hiyo inapunguza tuu maumivu na kama kuna mtu
anaudhibitisho kuwa inatibu alete ifanyiwe uchunguzi ili tubaini kama ni
kweli inatibu". Amesema.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile amesema kuwa
katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa
nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani
upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa
nchini.
"Ifahamike
kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na
saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo
mwaka 2020".Amesema.
0 comments:
Post a Comment