Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Serikali
imesema mtumishi anayefanya kazi katika Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) akibainika
kushiriki vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua mara moja.
Mkurabita
ilianzishwa kwa lengo la kumsaidia anayemiliki ardhi kimila atambulike
kisheria na apewe hati itakayomwezesha kupata mkopo ili aendeleze
biashara.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu
George Mkuchika alitoa onyo hilo alipotembelea taasisi hiyo. Alisema
asingependa kusikia kuna mwananchi anatafuta hati au wanataka eneo lake
lipimwe lakini mtumishi wa Mkurabita anamweleza kuwa ili kazi yako iende
haraka lazima ‘waonane’ jambo ambalo si sawa.
“Naomba
muelewe, anayepambana na rushwa ni Rais mwenyewe kwa sababu Takukuru
(Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa) ipo chini yake. Pia, Mkurabita
ipo chini ya Ofisi ya Rais Ikulu.
“Maana
yake Waziri wa Mkurabita ni Rais John Magufuli, mimi namsaidia kwa hiyo
mnapofanya kazi hapa mjue mkuu wa nchi ndiyo mwenye wizara,” alisema
Kapteni Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala Mjini (CCM).
Mratibu
wa Mkurabita, Seraphia Mgembe alisema licha ya mafanikio walionayo kuna
changamoto ya kutopata fedha za kutosha ili kujiendesha. Alisema mwaka
2009 Mkurabita iliomba Sh43 bilioni kwa ajili kufanya shughuli zake
kulingana na mpango kazi wao, lakini fedha walizopata hadi sasa ni
asilimia 55 sawa na Sh23 bilioni.
0 comments:
Post a Comment