Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na mhudumu wa kukata tiketi katika kituo cha Kivukoni wakati alipofanya ziara kuangalia namna abiria wanavyopata huduma zao, juu akikata tiketi ya kuingia ndani.
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake katika kivuko cha Kivukoni na Kigamboni na kujionea uendeshaji wa huduma bora kwa abiria kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na Mhandisi wa kivuko Ally Daudi na akipewa maelezo ya maendeleo ya vivuko vyote vilivyopo chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akikagua mashine za kieletroniki za tiketi zilizofungwa katika Kivuko cha Kigamboni na Kivukoni wakati wa ziara yake iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa amefanya
ziara katika kivuko cha Kigamboni na kujionea namna mashine mpya za
kieletroniki zilivyoweza kufungwa na kumtaka mhandisi aanze kuzifanyia
majaribio kabla ya mwaka huu kuisha ili Januari 2018 zianze kutumika.
Akizungumza
baada ya kumaliza ziara yake na kujionea namna wafanyakazi wanavyotoa
huduma kwa abiria wanaofika kwa ajili ya usafiri kwa kivuko kutoka
Kigamboni na Kivukoni, Naibu Waziri Kwandikwa
amesema kuwa amefurahishwa na huduma zinazotolewa na zaidi amezungumza
na baadhi ya wananchi na wote wameonekana kufurahishwa.
0 comments:
Post a Comment