Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya
uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya
TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China
(China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya
Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa
iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na
Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla
Vumilia (kushoto). PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG.
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo
ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi
waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -
CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia
ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao
umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni
Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi
kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi
zaidi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri akizungumza wakati wa hafla ya
kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya
TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa
ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association
of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China
nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA,
Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia
(kushoto) akitolea ufafanuzi wa masuala mbali mbali jinsi umoja wao
ulivyo na lengo kuu la kuweza kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya
treni ya TAZARA hasa wa kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.
Halfa hiyo iliyofanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akiingia ukumbini.
Vijana wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (mwenye
tai nyekundu) akiwa na Mwenyekiti wa China Alumni Association of
Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). Balozi wa China nchini
Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald
Phiri wakiwa katika picha ya pamoja na wanaumoja wa CAAT. Hafla hiyo
ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment