Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mazingira ya ndani yanaridhisha kutokana na usafi ambao
unazingatiwa sana na wahusika licha ya changamoto za hapa na pale.
Hawa ni wanaushirika wa Kisutu Poultry Farm Cooperative
Society (KIPOCOSO), ambao wamekuwepo katika soko hilo kwa zaidi ya miaka 28 na
ndio waanzilishi wa kuchinja kuku jijini Dar es Salaam.
Na Daniel Mbega,
MaendeleoVijijini.
SAUTI za kuku zinasikika hata ukiwa nje ya jengo dogo ndani
ya Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, lakini ghafla zinakoma na zinasikika
nyingine.
Siyo kwamba kuku hao wanahitaji chakula ama wanacheza, bali
hapa ni machinjio, na sauti zinapokoma ujue tayari zimekwishapigwa kisu na
zinaandaliwa kwa ajili ya kitoweo.
Nje ya jengo hilo unaweza kuwa umekuta akinamama wengi
wakiwa wamelundikana huku wakiwa wamekalia ndoo zao.Hawa nao wanasubiri huduma, wanataka kununua utumbo, miguu
pamoja na vipapatio vya kuku hao wanaochinjwa ili wakafanye biashara.
Akinamama hawa wanatoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar es Salaam na hapa Kisutu ndiko mahali pekee ambako wanaweza kupata bidhaa
hiyo wanayokwenda kuuza mitaani.Bila shaka baadhi yetu tumekutana ama tumewakuta akinamama
wakiuza firigisi na utumbo mitaani, basi amini kwamba asilimia kubwa wanapata
bidhaa hiyo katika eneo hili la Kisutu.
Ukiingia ndani ya jengo hilo usishangae ukasalimia
usiitikiwe na watu wengi, japokuwa waliomo ni wengi.Kabla hujajua usimame wapi, utasikia sauti ya mtu akikutaka
radhi kwamba anaomba kupita ama anataka kuweka mzigo.Naam. Kila mtu hapa yuko ‘busy’ na kazi inakwenda mtindo
mmoja, na hata kutokukuitikia si kwamba wanafanya kiburi ama hawajakuona, la
hasha. Kwa sababu wanataka kuhakikisha kazi wanayoifanya inakuwa katika hali
bora hasa ikizingatiwa kwamba hicho ni chakula kwa afya ya binadamu.
0 comments:
Post a Comment