Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akizungumza na katika uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akikabidhiwa mfano ufunguo wa jengo la mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) kutoka kwa Mratibu wa Miradi, Devis Shemangali unaofadhiliwa na Banki ya Dunia leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri
wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Suleiman Jaffo amewataka watendaji wa Manispaa ya Temeke kutoa
ushirikiano ili kuwezesha kukamilika kwa mradi wa Uendelezaji wa Jiji la
Dar es Salaam (DMDP) na watendaji watakaoshindwa kutoa ushirikiano huo
watashughulikiwa.
Akizungumza leo wakati uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) lililojengwa
katika Manispaa ya Temeke, Jaffo amesema mradi huo utawezesha manispaa
ya Temeke kuwa ya sura mpya na kuwa mfano kwa jiji la Dar es Salaam.
Amesema mradi utawezesha kujengwa kwa barabara na mifereji na hivyo kupunguza msongamano wa magari.
Amesema
mradi huo ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) utatekelezwa katika
jiji zima la Dar es Salaam katika kupanga mji kuwa na makazi bora yenye
huduma zinazoendana na makazi hayo.
“Temeke
mmekuwa na bahati ya kuwa ya kwanza kutekeleza mradi huu, shirikianeni
kuifanya Temeke kuwa ya kisasa kwa kuondoa Temeke iliyokuwepo zamani
isiyokuwa na miundombinu rafiki kwa makazi ya wananchi,” amesema.
Mratibu
wa mradi huo katika manispaa ya Temeke, Edward Simon amesema Shilingi
bilioni 265 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi barabara na mifereji. Amesema
jumla ya kilometa 91 za barabara za ndani zitajengwa kwenye manispaa
hiyo.
Amesema mradi huo ukikamilika utawezesha barabara kupitika na kupunguza mafuriko kutokana na kutengenezwa mifereji.
0 comments:
Post a Comment