Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) imeendesha mafunzo kuhusu
Mfumo wa Udhibiti wa Viashiria Hatarishi Mahala pa Kazi yanayofanyika
Ukumbi wa VETA mkoani Dodoma.
Mafunzo
haya ya siku nne yanajumuisha wakuu wa Idara, wakuu wa vitengo,
wakurugenzi wasaidi na wasimamizi wa udhibiti wa vihatarishi katika
sehemu ya kazi.
Akifungua
mafunzo hayo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii-
Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Marcel Katemba amesema kuwa suala la
udhibiti wa viashiria hatarishi linatokana na matakwa ya Sheria ya
Fedha za Umma ya mwaka 2001 (2010) na Waraka wa Hazina namba 12 wa
2012/2013 unaoitaka kila Taasisi ya Umma kuzingatia uandaaji na
utekelezaji wa Mfumo wa Menejimenti ya Viashiria vya Vihatarishi mahala
pa kazi.
“Mafunzo
haya ni nyenzo ya utumishi wa umma katika kudhibiti wa mifumo ya ndani
ya Taasisi na hivyo kuleta ufanisi katika shughuli na utendaji wa kazi
za kila siku na kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kiutendaji na za
fedha zenye kuaminika” alisema Bw. Katemba.
Kaimu
Katibu Mkuu Bw. Marcel Katemba amewakumbusha washiriki kuwa, mafunzo
hayo ni mwendelezo wa yale yaliyofanyika mwezi Julai, 2016, hivyo ni
jukumu la pamoja kati ya Menejimenti na watumishi wote wa Idara kuu ya
Mendeleo ya Jamii kwa ujumla wao kusimamia kikamilifu Viashiria
Hatarishi katika Idara na Vitengo husika.
Ameongeza
kuwa muendelezo huo utawaongezea uwezo watendaji, kuwa na uelewa wa
pamoja wa kutosha kuhusu viashiria vilivyo katika maeneo ya kazi.
Akitoa
mada katika mafunzo hayo, Mratibu Bw. Dickson Rusage amesema kuwa Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni miongoni mwa
Wizara tano (5) kati ya Wizara 21 za Serikali ambazo zimeweza
kuanzisha mfumo wa udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi na
kuutekeleza.
Ameongeza
kuwa Idara kuu ya Mendeleo ya Jamii imepiga hatua zaidi kwa kuwatumia
wataalam wake wa ndani katika kutoa mafunzo ya uelewa na kusimamia
udhibiti wa vihatarishi.
Bw.
Rusage amebainisha kuwa changamoto zilizopo katika kuendesha mfumo huo
ni pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha, mfumo kutopewa kipaumbele,
kutokuwepo dhamira ya dhati katika matumizi ya mfumo, kutozingatia mfumo
katika kufikia malengo ya Wizara, Idara, na Taasisi husika.
Kwa
upande wake Mwezeshaji katika Mafunzo hayo Bw. Moris Jackson amesema
kuwa manufaa ya mfumo wa udhibiti wa viashiria mahala pa kazi ni kuwa
Wizara inayokuwa na mfumo huu, wabia wa maendeleo wataiamini Taasisi
kwamba rasilimali zinazotolewa zitakuwa salama maana viashiria
vinafahamika na vimewekewa mifumo ya ufuatiliaji na udhibiti kwa manufaa
mapema.
Mada zitakazowasilishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Maana na makundi, Faida na Kanuni za Usimamizi wa Viashiria vya Vihatarishi, Matakwa
ya kisheria kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi nchini, Muundo na maeneo
muhimu ya kimwongozo, Mgawanyo wa majukumu katika Usimamizi wa
Vihatarishi na nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa kuandaa na
kusimamia Vihatarishi.
Mategemeo
ya mafunzo hayo ya mahala pa kazi yanalenga washiriki kuweza kubaini
vihatarishi ambavyo viliwekwa mwaka jana na sasa havitakiwi kuwepo tena,
kubaini vihatarishi vipya ambavyo ama vilisahaulika au vitaibuliwa sasa
kutokana na shughuli na kazi za Idara na Vitengo hasa baada ya mwaka
kuisha na kupata maoni na ushirikiano wa kutosha ili kwa pamoja kufikia
malengo yaliyokusudiwa katika kudhibiti viahatarisi kazini.
0 comments:
Post a Comment