Mkurugenzi
Mtendaji wa Reaching Out Destinies Foundation(RDF) Bi. Jane David
akifungua rasmi kwa maombi sherehe za kuwashukuru wadau wao kwa kuwa
nao kwa muda wa mwaka mzima, na baadae kutoa shukurani zake za dhati kwa
ushirikiano wao kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
Mkurugenzi
wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema akielezea historia ya asasi
hiyo,kuwa walianza wakiwa wa 3 lakini kwa sasa wapo zaidi ya 1300,na
kwa mwaka huu walifanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh milioni 1o ambazo
zimeweza kuwasaidia watu wenye makundi maalum wakiwemo yatima na wajane.
Mkurugenzi
wa Miradi ya nje na Mahusiano kutoka (RDF) Bi. Jackline Nicetas
akielezea namna asasi yao inavyofanya kazi pia kuwafikia watu mbalimbali
wenye uhitaji hasa wale waliopo majumbani, ambapo waliweza kuwaona
wajane 3 mkoani Dar es salaam na Mjane mmoja mkoani Pwani, pia wameweza
endesha semina,kuwa na camp na mentor ship forum
Bi
Josephine Mbago akitoa shukurani zake za dhati kwa RDF kwa kwenda mpaka
mkoani Pwani kumuona Mama yeke ambaye sasa ni Marehemu na kuwasaidia
kwa kile walichokuwa nacho, na kusema kuwa alijifunza kuwa 'hautakiwi
kuwa na elimu wala pesa ndio uweze kumasidia mtu bali talanta uliyokuwa
nayo ndio itakuwa msaada mkubwa kwa wengine', mwisho aliwaombea kwa
Mungu awazidishie zaidi pale palipo pungua.
Mwanadada
Pili Amani ambaye pia ni Mwimbaji akitoa ushuhuda wake namna RDF ilivyo
msaidia ambapo alisema kuwa unapompa mtu pesa bila kumpa moyo
haimsaidii, aliwashukuru sana kwa mambo waliyo mtendea na kuwaombea
waendelee kuwa na moyo huo. Alimalizia kwa kusema kuwa kumpenda mtu
ambaye haujawahi kuonana nae ni jambo la muhimu na Mungu anakubariki.
Mwanachama
wa RDF Bi. Frida Bariki akishukuru kwa yeye kukutanishwa na RDF ambapo
alisema kwake ulikuwa ni ushuhuda mkubwa ambapo amejifunza upendo,moyo
mkunjufu na kujitoa pia aliwaombea Mungu awape moyo wa unyenyekevu na
awape uwezo wa kutenda mambo makubwa zaidi
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati Ambrose Wankamba akitoa pongezi na
shukurani kwa asasi ya RDF kwa kuwatembelea ambapo waliweza
kuwabadilisha katika mambo mengi sana na kuwaomba wapate kuwatembelea
tena pindi watakapo pata nafasi.
Mwalimu
wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati Bi. Lightness Mamkue akitoa
shukurani zake za dhati kwa niaba ya shule yake kwa RDF ambapo
wamewafanyia mambo makubwa ambayo kwa moyo wa binadamu hawawezi kuyaona
lakini rohoni, ambapo pamoja na wao kuanza kuwalea wanafunzi kiroho
zaidi.
Afisa
Elimu Kata ya Mzinga , katika Manispaa ya Ilala Bi. Yusta Grant
alisisitiza kuwa pamoja na kuwasaidia watu kifedha au kwa vitu
mbalimbali pia ni muhimu kuongea nao na kuwapa moyo kama RDF wafanyavyo.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Mzinga, Manispaa ya Ilala Bw. Geral Salota akitoa
salam zake za Shukurani kwa RDF na kuahidi kuendelea kuwaombea kwa kazi
kubwa wanayoifanya.
Bi.
Saum Rashid kutoka Ulingo/Jumuia ya Wanawake , akitoa shukurani zake za
dhati kwa RDF kwa kuendelea kufanya vizuri katika kazi zao za
kuwasaidia wale wenye mahitaji na kuwasihi waendelee hivyo hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji (RDF) Bi. Jane David (kushoto) na
Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema (kulia) pamoja na wageni wengine (hawapo pichani) wakimuombea muongozaji wa kipindi cha Jukwaa la mazungumzo kinachoitwa 'Destinies Series' Bi.Jackline Nicetas (wa kati kati) kabla ya kipindi hakijaanza.
Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema (kulia) pamoja na wageni wengine (hawapo pichani) wakimuombea muongozaji wa kipindi cha Jukwaa la mazungumzo kinachoitwa 'Destinies Series' Bi.Jackline Nicetas (wa kati kati) kabla ya kipindi hakijaanza.
Mgeni
Rasmi katika sherehe za kutimiza mwaka mmoja wa RDF na ufunguzi wa
Jukwaa la mazunguzo la 'Destinies Series' Mchungaji Salome akizungumza
mambo mbalimbali ambapo baadhi ya mambo aliyoongelea ni pamoja na
kushindwa kujiandaa ama kusimamia vipaumbele vyako sahihi vinaweza
kuathiri hatma ya maisha yako.
'Talk Show' ikiendelea
Mwongozaji wa kipindi hicho Bi. Jackline Nicetas akiendelea kuchokoza mambo mbalimbali
Maombi mbalimbali yakiendelea
Wageni wakiwa wanasikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kutimiza mwaka mmoja wa RDF
Picha ya pamoja
Picha zote na Fredy Njeje
0 comments:
Post a Comment