Moto huo ukiendelea kuwaka.
MOTO mkubwa wa gesi umelipuka na kuteketeza nyumba eneo la Hospitali ya Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam jioni hii kutokana na Bomba la gesi kutoka Songo Songo, Lindi/Mtwara kwenda Ubungo, Dar, kupasuka na kusababisha moto mkubwa uliozua taharuki kwa wakazi na wafanyabiashara wanaozunguka eneo la Buguruni Mnyamani.
Taarifa za awali za zinasema bomba hilo limelipuka baada ya mafundi wa Dawasco waliokuwa wakichimba kwa ajili ya kupitisha mabomba yao ya maji, kulitoboa bomba hilo la gesi kimakosa.
Kikosi cha kuzima moto kimefika eneo la tukio na kinafanya kila juhudi za kuuzima moto huo ambao unaonekana kusambaa kwa kasi ambapo moto huo umesababisha magari na treni kushindwa kupita eneo hilo, chanzo kimedaiwa ni kupasuka kwa bomba la gesi.
Madhara yaliyosabaishwa na moto huo ni kuteketea kwa baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara, kuungua kwa nguzo za Tanesco na nyumba moja imeteketea kabisa lakini hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki dunia wala kujeruhiwa kutokana na moto huo.
Akizungumza na Global TV Online eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema wanendelea na juhudi kubwa ya kuzima moto huo na kwamba tayari wameshawasiliana na Kampuni ya Pan Africa ambao ndiyo ni wamiliki wa bomba hilo la gesi ili waweze kufunga valve ya sehemu ambako gesi hiyo inatokea (Mtwara), jambo ambalo litasaidia kuzuia kuendelea kutembea kwa gesi, hivyo kufanya urahisi wa kuuzima moto huo.
CHANZO:GPL
0 comments:
Post a Comment