Mrakibu
wa Magereza Kitengo cha Sheria, Absalom Mokiry akifafanua mambo mbali
mbali juu ya wafungwa na mahabusu waliopo mahakamani ikiwemo kuingiza
simu na vitu vilivyokatazwa gerezani kwa kutumia njia zisizostahili.
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
WAMETAFUTA
mbinu mbadala! Ndivyo unavyoweza kuelezea kinachoendelea kwenye baadhi
ya magereza yaliyopo nchini kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia
sehemu zao za siri kwa ajili ya kuingia na simu za mkononi pamoja na
sigara.
Sheria
za magereza kuna baadhi ya vitu vimepigwa marufuku ikiwamo simu ya
mkononi, dawa za kulevya, visu ,nondo na sigara lakini baadhi ya
mahabusu na wafungwa wamekuwa wakiingia nazo kwa kutumia mbinu
mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Mrakibu Msaidizi wa Magereza, makao makuu kitengo cha sheria
Absalom Mokily ameiamba Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu
yaliyofanyika leo alipokuwa kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria
inayoendelea jijini Dar es Salaam kuwa kuna mbinu nyingi wanazozitumia
mahabusu na wafungwa kuingia na vitu hivyo.
SEHEMU ZA SIRI ZINATUMIKAJE? IKO HIVI .
Akielezea
zaidi kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri
kuingia na vitu ambavyo vimepigwa marufuku , Mokiry amesema wenye tabia
hiyo wamekuwa wakijaza mizigo kupitia njia za haja kubwa na njia ya
mkojo.
Amesema
kuwa wanaoingia na vitu hivyo hata askari Magereza wanashindwa kubaini
kutokana na utaalamu wanautumia kificha vitu hivyo vilivyopigwa marufuku
kuingizwa magerezani.
"Unaweza
kuwapekua na usione chochote, hivyo unapomruhusu aondoke, anachokifanya
anakwenda chooni na kisha kutoa vitu alivyoficha kwenye sehemu zake za
siri,"ameeleza.
Mokily
amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Magereza namba 149 ya mwaka
2003 imezuia baadhi ya vitu kuingizwa magerezani.Ametaja baadhi ya vitu
hivyo ni ni silaha, simu, visu, nondo, bangi, tumbaku na simu za
mkononi."Ni marufuku kuingia na vitu,"amesema.
Amesema
kuwa tabia hiyo si tu kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu wa kiume tu
bali hata wanawake nao wanatabia hiyo kwa kuchukua vitu hivyo na kuficha
sehemu zao za siri.
"Wanawake
wenye tabia ya kuficha vitu wanachokifanya ni kukimbilia chooni na
kisha huvitoa na baada ya hapo utashangaa kuona wanawasiliana na watu
walioko nje kwa kutumia simu ambazo wameingia nazo kwa mtindo
huo,"amesema.
Amefafanua
kuna watu magerezani wamekuwa wakiingia na kutoka , wengine wazoefu
magerezani hasa mahabusu.Wanapokwenda mahakamani inakuwa ndio njia ya
wao kupata vitu hivyo na kisha kuingia navyo magarezani.
WASHINDWA KUTHAMINI UTU WAO
Wakati
huohuo, Mokiry anasema mfungwa anachukuliwa kama binadamu na kubwa
zaidi askari magereza wanathamini sana utu wa watu wote lakini baadhi ya
wafungwa na mahabusu wameshindwa kuthamini utu wao hasa wakiwa
magerezani.
"Unapawakagua
huoni chochote lakini ukienda chooni utagundua wameingia na pakiti za
sigara na simu na vitu vingine ambavyo haviruhusiwi.Tunashindwa
kuwapekua sana kwani unaweza kuambiwa unadhalilisha utu wa mtu lakini
wenyewe wamekuwa wakwanza kutothamini utu wao,"amesema.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA
Mokiry
ameongeza mahabusu au mfungwa atakayekamatwa akiwa na vitu hivyo
huchukuliwa hatua za kisheria ikiwamo ya kupelekewa mahakamani na
ikitokea kuna mtumishi asiye mwaminifu na anayekiuka kanuni huchukuliwa
hatua na ikiwezekana anafukuzwa kazi ikibainika ni kweli amehusika
kusaidia kuinga kwa vitu hivyo.
MIMBA GEREZANI
Kwa
upande wa Mrakibu wa Magereza, Amina Kavirondo alipoulizwa kuhusu
baadhi ya wafungwa na mahabusu kupata mimba wakiwa magerezani, amejibu
haijawahi kutokea mwanamke akapata ujauzito akiwa gerezani.
"Kinachotokea
wapo baadhi ya mahabusu na wafungwa wanaoingia wakiwa na mimba gerezani
na hivyo hujifungulia huko huko na kupata watoto,"amesema.
Amefafanua
wafungwa na mahabusu wanawake wanaipongia gerezani wanapimwa afya ili
kubaini hali zao na kama mjamzito ripoti hupelekwa Makao Makuu ya
Magereza na usimamizi wake kuanzia mwanzo hadi mwisho.
"Mfungwa
wa kike akibainia ni mjamzito humpokea na kumtunza ili kuhakikisha
anakuwa salama yeye na kiumbe kilicho tumboni mpaka pale atakapojifungua
salama,"amesema Kavirondo.
MICHUZI BLOG
0 comments:
Post a Comment