TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
· Mustafa Hassanali amealikwa katika hekalu la Buckingham
· Kampuni ya Rwanda Air kumsafirisha Mustafa Hassanali kuelekea uingereza.
· Nguli wa mitindo barani Afrika, Mustafa Hassanali amealikwa katika shughuli ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola.
Nguli
wa mitindo barani Afrika ambaye ametunukiwa tuzo mbalimbali, Mustafa
Hassanali, ameweza kukamata jicho la familia ya kifalme, Nguli huyo wa
mitindo atakuwa mgeni moja wapo kati ya wabunifu wengine wa kimataifa
kutoka nchi mbalimbali za jumuiya ya madola, watakaoshiriki katika
shughuli ya kifahari kuhusu mitindo, katika hekalu la malikia wa
Uingereza huku wakisherekea ubora wa kazi za ubunifu.
Mustafa Hassanali amepokea mwaliko ambao
haukutarajiwa unaomtaka kushiriki katika sherehe ya kubadilishana
mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola itakayofanyika
katika hekalu la Buckingham tarehe 19 mwezi huu, mbele ya uwepo wa
Catherine Elizabeth Mountbatten-Windsor (Kate Middleton) na Sophie Countess of Wessex amabo ni mabint kutoka familia ya kifalme.
“Ni heshima kubwa na
ufahari kualikwa katika sherehe hii ya kifahari ikayofanyika katika
hekalu la Buckingham kwa amri ya Malikia na kuweza kusherekea nae kazi
za mitindo kutoka nchi zote za jumuiya ya madola, hii inaonyesha kuwa
kazi yako na kujitolea katika sekta ya mitindo ya Tanzania inakubaliwa
na kutambuliwa kimataifa.” Alisema Mustafa Hassanali.
Aliongeza
kuwa “ Nashukuru kwamba , kwa miaka mingi nimeleta mabadiliko mabayo
nilitamani kuyaona katika sekta ya mitindo ya hapa nchini, kama Rais wa
Marekani Marehemu John F Kennedy alivyosema, usiulize nini nchi yako
inaweza kukufanyia, jiulize nini unaweza kufanya kwa nchi yako.kwa miaka
kumi iliyopita nilianzisha na kuandaa jukwaa kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati lijulikanalo kama Swahili Fashion Week, na hivi karibuni ni nimekuwa mwanachama mwanzilishi na
mwenyekiti wa Kampuni ya kukuza kazi za mitindo na ubunifu hapa nchini
(Fashion Association of Tanzania) ambacho kina nia ya kujenga na
kuimarisha vipaji na sekta ya mtindo ya Tanzania.
Mchango
wa Mustafa Hassanali katika sekta ya mitindo nchini Tanzania na Afrika
kwa ujumla haujaenda bure, shirika la ndege ya kitaifa ya Rwanda,
imewezesha safari ya Mustafa iliapate uzoefu wa ndoto ya kusafiri kutoka Afrika hadi mji wa Gatwick nchini Uingereza kupitia ndege yao ya mfululizo wa A330-300.
“Ni
heshima kubwa na tunajivunia kuweza kumsafirisha nguli wa mitindo
Mustafa Hassanali aweze kuhudhuria sherehe ya mitindo iliyoandaliwa kwa
nchi za jumuiya ya madola itakayofanyika katika hekalu la Buckingham.
Vilevile ndege zetu zinasafilisha mara mbili kwa siku kutoka Dar es
Salaam hadi Kigali na miji mingine 23 kutoka Kigali na nchi nyingine
zaidi” alisema Meneja wa Rwanda Air nchini Tanzania, Bw.Ibrahim Bukenya.
Sherehe
hiyo ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya
madola, zitakuwa na wabunifu 52 na wataalamu wa sanaa za mikono kutoka
nchi tofauti za jumuiya ya madola, wataungana kutengeneza nguo moja ya
kipekee na endelevu, ambayo itaonyeshwa katika sherehe hiyo
itakayofanyika katika hekalu la Buckingham, huku nguo hiyo ikiwa na
lengo kutumia jumuiya ya madola pamoja na nafasi ya biashara ya mitindo
ya wataalamu wa sanaa za mikono inaweza kuleta matokeo chanya katika
kuwawezesha wanawake na kupunguza umasikini.
0 comments:
Post a Comment