Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi, (kulia), akipeana mikono na Meneja Mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari makao makuu ya TPB jijini Dar es Salaam Februari 16, 2018.BENKI
ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF),
kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja. Mradi huo unaoitwa
“Digitalizing Informal Savings Mechanisms”
NA K-VIS BLOG/Khalfan
Said
BENKI
ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF),
kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja. Mradi huo unaoitwa
“Digitalizing Informal Savings Mechanisms” utaendeshwa kwa kipindi cha miaka
mitatu (3) ambapo TPB inatarajia kuwaunganisha kwenye mfumo rasmi wa kifedha
wateja wapya laki Mbili na nusu hadi kufikia mwaka 2020, Afisa Mtendaji Mkuu wa
TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo Februari 16, 2018.
Kitangaza
mradi huo mbele ya waandisahi wa habari, Bw. Moshingi alisema, mradi huo
utaanzia Mkoa wa Ruvuma, na baadae kupelekwa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Njombe,
Iringa na Morogoro.
“Watanzania
wengi waishio kwenye mikoa ya pembezoni, hususani wenye vipato vidogo
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma za kifedha. Kupitia
ushirikiano huu na SatF, TPB itawawezesha wananchi kupitia makundi au mtu mmoja
mmoja, kujiwekea akiba kupitia teknolojia rahisi na salama isiyowalazimu kwenda
kwenye tawi la benki ili kupata huduma hizo za kifedha. Njia hii itawawezesha
wananchi kutatua changamoto zao mbalimbali za kifedha na pia kuwaingiza kwenye
mfumo rasmi wa kiuchumi.
Akifafanua
zaidi Bw. Moshingi alisema, Benki ya TPB ni benki ya kwanza hapa nchini
kuanzisha utoaji wa huduma za kibenki kwa makundi kupitia simu za mkononi,
maarufu TPB POPOTE. Hivi sasa, wateja kupitia vikundi vyao wanaweza kuweka
akiba na hata kukopa kupitia simu zao za mkononi.
Kwa
upande wake, Meneja wa mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey,
amesema benki ya TPB ndio benki ya kwanza kufanya kazi na taasisi yake hapa
nchini, na walivutiwa na namna ambavyo TPB imeonyesha dhamira ya dhati ya
kuwasaidia wananchi hao kupata huduma za kifedha.
Pia,
amesema taasisi yake inayo furaha kubwa kupata nafasi ya kufanya kazi na benki
ya TPB , taasisi ya fedha yenye sifa na historia ndefu katika jitihada za kupeleka huduma za kifedha
kwa wananchi wake popote walipo. Hii ni fursa nzuri kwa SatF na TPB kujenga
umoja imara utakaowawezesha kuwafikia wananchi maskini.
“SatF
ni programu maalum yenye malengo ya kuhakikisha huduma za kifedha za uhakika
zinawafikia wananchi wengi walio nje ya mifumo rasmi ya kibenki, programu hii
inaratibiwa na shirika la Oxford Policy Management kwa ufadhili wa taasisi ya
kimataifa ya MasterCard Foundation, dhumuni kuu ikiwa ni kuboresha upatikanaji
wa huduma za kifedha kwa wananchi na jamii zenye vipato vya chini kwenye nchi
zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara.” Alifafanua Bw. Peachey
Aidha
Bw.Peachey aliendelea kwa kusema kuwa lengo kuu la SatF ni kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata huduma endelevu za kifedha, na kwa sababu hiyo, wapo tayari
kushirikiana na benki ya TPB kwa kutoa msaada wa kifedha na kiufundi.
“Tunaamini
kuwa jitihada tunazofanya zitakuza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa
wananchi ambao hapo awali walitengwa na huduma hizi, na hivyo kukuza uwezo wao
kiuchumi”, alisema.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya Finscope mwaka 2017, asilimia 59 ya
Watanzania wanavipato vya msimu, na miongoni mwa changamoto zinazowakabili
kubwa ni pamoja na uwezo wa kumudu gharama za matibabu, na malipo ya ada za
shule kwa ajili ya watoto wao. Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 40 ya
Watanzania hukopa fedha kutoka kwa jamaa ama rafiki kwa ajili ya kutatua
changamoto mbalimbali za kifedha zinapojitokeza. Kiasi cha Watanzania Milioni
7.8 wametengwa na huduma za kifedha, na hili limeleta uhitaji mkubwa wa
mazingira bora ya kuwawezesha wananchi hao kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba
ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Meneja wa mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey(kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Bw. Sabasaba Moshingi.
Meneja Mkuu, anayeshuhughulikia masuala ya Kampuni ya TPB Bank, Bi. Noves Moses, akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo.
Bw. Moshingi, na Bw.Peachey, wakiwa na maafisa wa TPB Bank, na SatF.
Maafisa wa TPB wakisikiliza
Bw. Moshingi akifafanua jambo huku Bw. Peachey, (wakwanza kushoto), na Bw.Ignas Jacob kutpoka SatF, wakisikiliza.
Maafisa wa TPB, wakiwa kwenye mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment