KFS Tanzania imetangaza rasmi leo kuwa ndio kituo pekee nchini kitakachorusha matangazo ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 (FiFA World Cup 2018) bure inayotarajiwa kuanza tarehe 14 Juni 2018 na kumalizika tarehe 15 Julai 2018 nchini Urusi.
KFS Tanzania wakishirikiana na kituo cha Televisheni cha TBC watarusha matangazo hayo moja kwa moja.
Kutakuwa na mechi 32 zikiwemo zote zitakazochezwa na timu za Afrika, Robo Fainali, Nusu Fainali pamoja na Mechi za mwisho ya Fainali,hii si ya kuikosa hata kidogo.
KFS inapatikana kupitia King'amuzi cha Startimes Chanel 103, Continental Chanel namba 07 na Ting Chanel namba 36
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba(Kulia) akisaini Mkataba wa makubaliano kati ya KWESE free Sports (TV1) na TBC kuonesha Kombe la Dunia kuanzia Juni 14,2018
Mkurugenzi wa KWESE free Sports (TV1) Bw. Joseph Sayi(kushoto) akisaini Mkataba wa
makubaliano kati ya KWESE free Sports (TV1) na TBC kuonesha Kombe la
Dunia kuanzia Juni 14,2018
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba pamoja na Mkurugenzi wa KWESE Free Sports Tanzania (TV1) Bw. Joseph Sayi wakipeana Mikono baada ya kusaini mkataba wa makubaliano kuonesha Mubashara Kombe la Dunia 2018, Buree bila kulipia.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba pamoja na Mkurugenzi wa KWESE Free Sports Tanzania (TV1) Bw. Joseph Sayi wakionesha waandishi wa Habari Mkataba waliosaini kushirikiana kuonesha Kombe la Dunia 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba akitoa neno wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari baada ya kuasini mkataba kati ya KWESE Free Sport Tanzania(TV1) na TBC kuonesha Kombe la Dunia mwaka 2018
Mkurugenzi wa KWESE Free Sport
Tanzania(TV1) Bw. Joseph Sayi akitoa neno wakati wa Mkutano na
waandishi wa Habari baada ya kuasini mkataba kati ya KWESE Free Sport
Tanzania(TV1) na TBC kuonesha Kombe la Dunia mwaka 2018
Meneja Masoko wa TBC Bi. Daphrosa Kimbory akiwasisitiza wafanyabiashara na watu mbalimbali kutumia fursa ya Kombe la Dunia kujitangaza na kuonesha bidhaa mbalimbali wakati wa kurushwa moja kwa moja kwa mashindano ya Kombe la Dunia 2018 (FIFA World Cup 2018)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TBC Bi. Edna Rajabu akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni za urushaji mechi kombe la Dunia 2018
Meneja Masoko wa KWESE Free Sport
Tanzania(TV1) Bi. Gillian Rugumamu, akiwahakikishia watanzania kuwa KWESE Free Sport Tanzania (TV1) pamoja na TBC watawaletea Burudani ya Kombe la Dunia Mubashara tena Buree na kwa Kiswahili hivyo waondoe wasi wasi wa kuwaza kulipia King'amuzi maana kutakuwa hakuna makato yoyote.
Mbunifu na Uzalishaji wa Vipindi kutoka KWESE Free Sport
Tanzania(TV1) Bw. Walter, akiwahakikishia watananzania kuwa kutakuwa na Studio mahili za utangazaji zenye watu mahili ambao watachambua Mechi zote za Kombe la Dunia 2018, hatua kwa hatua na kurushwa Mubashara bila Chenga.
Meneja Mkuu wa KWESE Free Sport
Tanzania(TV1) Bw. Mgope Kiwanga akizungumza neno wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari
Mhariri wa vipindi vya Michezo kutoka TBC Bw. Enock Mbwigane akitoa neno baada ya kumaliza mkutano pamoja na waandishi wa Habari
Picha na Blogs za Mikoa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment