Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WASHIRIKI WARSHA YA TGNP DAR LEO

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WASHIRIKI WARSHA YA TGNP DAR LEO


Washiriki wa warsha ya  wahariri Bw Karugeno ,Mohamed na Meena  wakiwa  katika warsha
Bw  Deo  Temba  kutoka  TGNP  aki
Mmiliki  wa  The Habari Blog Joachimu Mushi (kushoto) akifuatilia warsha  hiyo
Bi Kenny Ngomuo akitoa maelezo ya msingi katika  warsha  hiyo
kaimu  mkurugenzi  wa  TGNP Mary Nsemwa (kualia ) akifungua mafunzo  hayo leo

 Wahariri wa vyombo vya habarini nchini wametakiwa kuendelea kushirikiana na wanahabari ili kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa jamii katika mchakato wa utoaji wa maoni ya katiba mpya yenye mtazamo wa kijinsia.

 Rai hiyo imetolea leo na kaimu mkurugenzi wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Mary Nsemwa wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini katika ukumbi wa Hotel ya Courtyard iliyopo Upanga.

 Amesema kuwa wahariri wa vyombo vya habari wanaowajibu wa kuendelea kutua elimu kwa umma hasa katika kipindi hiki cha ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya ili kuweza kuipata katiba yenye mtazamo wa kijinsia zaidi .

 Hivyo amewataka wahariri kuhakikisha wanapigania haki za msingi kuingizwa katika katiba mpya ijayo .

Hata hivyo amesema kuwa wao katika TGNP wanaendelea kupongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na vyombo vya habari hapa nchini katika kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuibuka mambo mbali mbali hasa ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa miji.

 Nsemwa amesema kuwa ni lazima wahariri wa vyombo vya habari na wanahabari nchini kuendelea kupigania haki za watanzania ambazo zimeporwa na wachache ama kuendelea kuwanufaisha wachache ili ikiwezekana uchumi wa Taifa hili kuwanufaisha watanzania wote

Amesema kuwa suala la mabadiliko katika Taifa hili hayataletwa na mtu mmoja wala taasisi moja ila inahitaji kuwepo kwa ushirikiano mpana kwa jamii nzima. Kwa upande wake Prof Ruth Meena amesema kuwa katiba ya sasa inatoa haki kwa upande mmmoja na kuipokonya tena haki hiyo hivyo bado katiba inashindwa kueleweka vema kwa maslahi ya Taifa.
Na Francis Godwin

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa