Washiriki wa warsha ya wahariri Bw Karugeno ,Mohamed na Meena wakiwa katika warsha |
Bw Deo Temba kutoka TGNP aki |
Mmiliki wa The Habari Blog Joachimu Mushi (kushoto) akifuatilia warsha hiyo |
Bi Kenny Ngomuo akitoa maelezo ya msingi katika warsha hiyo |
kaimu mkurugenzi wa TGNP Mary Nsemwa (kualia ) akifungua mafunzo hayo leo
Wahariri wa vyombo vya habarini nchini wametakiwa kuendelea kushirikiana na wanahabari ili kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa jamii katika mchakato wa utoaji wa maoni ya katiba mpya yenye mtazamo wa kijinsia.
Rai hiyo imetolea leo na kaimu mkurugenzi wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Mary Nsemwa wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini katika ukumbi wa Hotel ya Courtyard iliyopo Upanga.
Amesema kuwa wahariri wa vyombo vya habari wanaowajibu wa kuendelea kutua elimu kwa umma hasa katika kipindi hiki cha ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya ili kuweza kuipata katiba yenye mtazamo wa kijinsia zaidi .
Hivyo amewataka wahariri kuhakikisha wanapigania haki za msingi kuingizwa katika katiba mpya ijayo .
Hata hivyo amesema kuwa wao katika TGNP wanaendelea kupongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na vyombo vya habari hapa nchini katika kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuibuka mambo mbali mbali hasa ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa miji.
Nsemwa amesema kuwa ni lazima wahariri wa vyombo vya habari na wanahabari nchini kuendelea kupigania haki za watanzania ambazo zimeporwa na wachache ama kuendelea kuwanufaisha wachache ili ikiwezekana uchumi wa Taifa hili kuwanufaisha watanzania wote
Amesema kuwa suala la mabadiliko katika Taifa hili hayataletwa na mtu mmoja wala taasisi moja ila inahitaji kuwepo kwa ushirikiano mpana kwa jamii nzima. Kwa upande wake Prof Ruth Meena amesema kuwa katiba ya sasa inatoa haki kwa upande mmmoja na kuipokonya tena haki hiyo hivyo bado katiba inashindwa kueleweka vema kwa maslahi ya Taifa.
Na Francis Godwin
0 comments:
Post a Comment