Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Dk Asha-Rose Migiro awa Balozi Uingereza

Dk Asha-Rose Migiro awa Balozi Uingereza

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Dk Asha-Rose Migiro
RAIS John Magufuli amemteua Dk Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu jana mjini Dodoma, Dk Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Migiro ataapishwa leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Dk Migiro aliteuliwa kuwa Balozi Februari 15, mwaka huu pamoja na wenzake wawili ambao ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi la Taifa (NSSF), Dk Ramadhani Dau.
Dk Migiro amewahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Nne na pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).
Katika Awamu ya Nne, aliongoza Wizara za Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Katiba na Sheria.

Chanzo Gazeti la Habari leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa