RAIS John Magufuli amemteua Dk Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu jana mjini Dodoma, Dk
Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe
ambaye amerudishwa nyumbani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Migiro ataapishwa leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Dk Migiro aliteuliwa kuwa Balozi Februari 15, mwaka huu pamoja na
wenzake wawili ambao ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi la
Taifa (NSSF), Dk Ramadhani Dau.
Dk Migiro amewahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika Serikali ya
Awamu ya Nne na pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).
Katika Awamu ya Nne, aliongoza Wizara za Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Katiba na
Sheria.
Chanzo
Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment