Home » » Airtel yawatangaza washindi wa "Nani Mkali" promosheni

Airtel yawatangaza washindi wa "Nani Mkali" promosheni


Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi. Jane  Matinde  akitanzanga washindi wa  promosheni ya Mkali nani kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) ambapo washindi wa siku hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kulia ni Afisa mawasiliano wa kampuni ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akishuhudia  tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini Dar-es-Salaam.
Afisa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi. Dangio  Kaniki akiongea na  waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza washindi wa  promosheni ya Mkali nani ambapo washindi wa siku hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki hujinyakulia  kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano  wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia  tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini Dar-es-Salaam.

===============  ===============  =========
 Airtel yawatangaza washindi wa "Nani Mkali" promosheni

*         Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki atangazwa

 
29, March 2012 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewatangaza washindi wa wiki hii ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo washindi wa kila siku watakabidhiwa shilingi milioni moja kila  mmoja na mshindi wa wiki ataondoka na shilingi milioni tatu. Washindi hao wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Arusha, Zanzibar, Dar es Salaam, Nzega - Tabora na Manyara

Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel
Dangio Kaniki alisema" Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania
kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa
washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali.  Na leo napenda kuchukua fulsa hii kuwatangaza washindi wa wiki hii ambao ni




KAANAEL LEMLE KANUYA

ARUSHA


50

          1,000,000.00

RAKESH MANSUR DEYAL


ZANZIBAR


34

          1,000,000.00

NAPEGWA DAVID MONGO


DSM


58

          1,000,000.00

MARIAM WAZIRI HAMISI


DSM


32

          1,000,000.00

GUVANTRAI SACHDEV SHANTILAL


ARUSHA


54

          1,000,000.00

YUSUPH NOHAI ANNAI


MANYARA


35

          1,000,000.00

YUSUPH  MATHIAS MANONI


NZEGA-TABORA


25

          3,000,000.00
Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha
washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Dangio

 kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.                                                        

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa