Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Usambazi wa Nishati Umeme nchini Tanzania (TANESCO) Bw. William Mhando (kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusiana na hali ya umeme katika gridi ya taifa. Katika ufafanuzi huo amesema mitambo ya kuzalisha umeme iliyounganishwa katikagridi ya Taifa ina uwezo wa kuzalisha jumla ya MW 1270.74, wakati mahitaji ya juu ya grid ya taifa ni yalifikia MW 829.58.katika robo ya kwanza ya mwaka ya mwaka 2012. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi.
Na.MO BLOG TEAM
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Usambazi wa Nishati Umeme nchini Tanzania (TANESCO) Bw. William Mhando amesema sababu ya kukatika kwa umeme hivi karibuni siyo mapungufu ya uwezo wa kuzalisha umeme, bali ni matatizo ya miundo mbinu ya kusambaza na kuzidiwa nguvu.
Amesema matatizo hayo yajitokeza zaidi katika mikoa ya Dar es Salaam na kuwa anapenda kutoa taarifa kuwa yalisababishwa na kuungua kwa transfoma zilizo katikati ya mji.
Pamoja na mambo mengine Bw. Mhando amesema mitambo inayozalisha umeme wa bei nafuu inapewa kipaumbele katika kuzalisha na mitambo yenye kuzalisha umeme kwa gharama kubwa kama mitambo ya kukodi inatumika kwa nafasi ya mwisho kama umeme mwingi zaidi unahitajika.
Habari kwa hisani ya Mo Blog
0 comments:
Post a Comment