Home » » HOT Nuuz: Wasanii wagomea Jukwaa la Sanaa Leo

HOT Nuuz: Wasanii wagomea Jukwaa la Sanaa Leo

 Viongozi wa Jukwaa la sanaa wakiwa katika mkutano 
 Mmoja wa Viongozi akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano huo 
Wakiendelea na Mkutano huku viongozi wengine wakisikiliza kwa umakini 
Na Mwandishi wetu maalum
Kiongozi wa BASATA na mwakilishi wa COSOTA bwana James Kagenge aliye mwakilisha mtendaji mkuu wa COSOTA bwana Nkinga amekutana na wasanii na wadau wa sanaa katika Jukwaa la sanaa Leo.
Katika mkutano huo ambao hufanyika kila Jumatatu eneo hilo, Wasanii na wadau wamelalamika kitendo cha COSOTA wamewajia juu Chama hicho Baada ya kuja na mada ya kuanzisha Tovuti ya mawasiliano kwa wasanii badala ya kuzungumzia mada iliyo kuwa imepangwa ambayo ilikuwa ni Mahuisho ya Haki Miliki na Haki shiriki na sheria yake. 
Pia katika mkutano huo wadau hao na wasanii wamelalamikia kitendo cha Viongozi hao kufika eneo hilo pale wanapo Jisikia kitendo ambacho hakioneshi picha nzuri.
Hata hivyo mwakilishi wa mtendaji Mkuu wa BASATA Mama Vicky Temu aliahirisha shuguri za jukwaa la sanaa na wadau hao walianza kutawanyika. Hata hivyo viongozi wa COSOTA waliwasihi waludi ili wapate kutoa ufafanuzi juu ya mambo ambayo walipanga kuyaongea lakini wasanii na wadau hao waligomea na hawakuwa tayali kujadili maswala hayo.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa