Home » » MCHEZAJI PATRICK MAFISANGO ATIMULIWA SIMBA

MCHEZAJI PATRICK MAFISANGO ATIMULIWA SIMBA






SIMBA imemtimua kiungo wake wa Kimataifa Patrick Mafisango kutokana na utovu wa nidhamu.

Mafisango
ambaye amekuwa akipewa onyo mara kwa mara na uongozi kutokana na tabia
yake ya ulevi, alirudia tena kitendo hicho hivi karibuni wakati timu
yake ikiwa kambini.


Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana toka kambi ya Simba iliyopo Bamba
Beach, Mafisango baada ya kuwa 'tungi' aliporejea kambini alitoa lugha
chafu kwa meneja wa timu hiyo Nichoalus Menard Nyagawa pamoja na kocha
mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic kabla ya taarifa kufika kwa uongozi na
ndipo mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage kuagiza atimuliwe.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa