Home » » MAWAKALA WA REDDS MISS TANZANIA WAPIGWA MSASA KABLA YA KUANZA KWA SHINDANO HILO

MAWAKALA WA REDDS MISS TANZANIA WAPIGWA MSASA KABLA YA KUANZA KWA SHINDANO HILO





Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao pia ni
Waandaaji wa Redds Miss Tanzania 2012, Hashim Lundenga akifungua rasmi
semina ya mawakala wa Miss Tanzania 2012 jijini Dar es Salaam iliyoanza
leo kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View ya Mbezi jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, kutoka Kampuni ya Bia ya
Tanzania (TBL) Victoria Kimaro na Salha Israel Miss Tanzania 2011.
 Washiriki wa semina hiyo wakiwa tayari
kupata maelekezo mbalimbali kutoka kwa waandaaji pamoja na wadhamini wa
shindano la Redds Miss Tanzania 2012.
 Albert Makoye Mkuu wa Itifaki kutoka
kamati ya Miss Tanzania akitoa mada katika semina hiyo iliyoanza leo
kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam.

Mawakala
wa Kamati ya Miss Tanzania kutoka mikoa mbalimbali na kanda wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa semina hiyo
leo jijini Dar es salaam.
Lundenga amesema  kuwa Kamati hiyo kupitia wadhamini, mwaka huu wamedhamiria
kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya Urembo nchini na waandaaji
pia wamedhamiria kupata warembo bora watakao shiriki shindano hilo la
urembo mwaka huu.

Lundenga pia alitoa kaulimbiu ya mashindano hayo kwa mwaka huu kuwa ni “MSHINDI BORA, MWAKILI BORA MWENYE SIFA BORA”

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa