Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili ya mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na REPOA katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam, leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akimpongeza Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Phillip Mpango kwa mada nzuri. Katikati yao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt. Ad Koekkoek.
Profesa Do Duc Dinh, kutoka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake ilivyofanikiwa kuondoa umaskini wakati wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini nchini Tanzania.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt. Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti, leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Profesa Ibrahim Lipumba, baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini, nchini.
0 comments:
Post a Comment