Mwenyekiti wa Tume wa Ufuatiliaji tatizo la Umeme katika Soko la Mchikichini, Mussa Kitakuru Kweka (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Wanaharakati wa Soko la Mchikichini, Godwin Kaison Ndabazi na Mfanyabiashara wa Mchikichini, Zabibu Ally Lukuba. Wafanyabiashara hao wamemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwapatia eneo la wafanyabiashara ndogo ndogo katika Soko hilo na limeweza kuwapatia ajira ya zaidi watu 10,000 aidha Soko hilo limekosa umeme kuanzia Disemba 13/2011 hadi leo kutokana na kutolipa deni la Milioni 230/- ambalo wamedai limesababishwa na Uongozi wa soko hilo.

Mwenyekiti wa Wanaharakati wa soko la Mchikichini Godwin Kaison Ndabazi (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 21.12, kuhusu matatizo yanayowakabili ya kukosa umeme pamoja na matatizo ya viongozi wa soko la Mchikichini katika Manispaa Ilala . Kulia ni Mwenyekiti wa Tume wa Ufuatiliaji tatizo la Umeme Sokoni hapo, Mussa Kitakuru Kweka.
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
0 comments:
Post a Comment