Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limepatwa na tatizo la kuanguka kwa nguzo 22 za umeme eneo la Kipawa – uwanja wa ndege jijini DSM kulikosababishwa na upepo mkali uliovuma kutoka eneo linalojengwa uwanja wa ndege wa Mwl, J.K. Nyerere.
Tatizo hilo la dharura litasababisha baadhi ya maeneo yote ya kipawa – Tandika na maeneo ya Temeke kukosa umeme wakati mafundi wa TANESCO wakifanya kazi usiku kucha.
Njia hiyo ya msongo wa kilovolti 33 unatarajiwa kurudishwa kwenye hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.
Shirika linawaomba wateja wake wote kuwa watulivu wakati mafundi wanahangaika na linatoa tahadhari kwa mtu yeyote kutogusa waya uliodondoka chini.
Uongozi wa Shirika uanaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa raia na wateja wake kwa ujumla.
Picha kwa Hissani ya Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment