Home » » RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BALOZI RAPHAEL LUKINDO.

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BALOZI RAPHAEL LUKINDO.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Balozi Raphael Lukindo huko Sinza jijini Dar es Salaam aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jumanne tarehe 27 Machi na kuzikwa Ijumaa tarehe 30 Machi katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dare s Salaam.Marehemu Balozi Lukindo aliyestaafu Mwaka 1988 aliitumikia serikali katika balozi mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Japan,Urusi,Poland,Hungary na Czechoslovakia.Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bibi Tereza Mvaa Lukindo,mke wa marehemu Balozi Raphael Lukindo wakati Rais Kikwete alipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza jijini Dar es Salaam kuwapa pole ndugu na jamaa kutokana na kifo cha Balozi huyo aliyezikwa juzi Ijumaa katika makaburi ya Kinondoni.
(picha na Freddy Maro).

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa