Home » » UWT TAWI LA MAKAO MAKUU YA CCM LUMUMBA WAPATA VIONGOZI WAPYA

UWT TAWI LA MAKAO MAKUU YA CCM LUMUMBA WAPATA VIONGOZI WAPYA




Mary Nchimbi ameibuka kuwa Mwenyekiti wa mpya wa tawi hilo



 
Mary akipongezwa na mgombea mwenzake wa Uenyekiti Sheila Luckisasi baada ya matokeo
Angela akimpongeza Mwenyekiti mpya Mary Nchimbo baada ya matokeo
 Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo wa uchaguzi kwenye ukumbi wa
Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es
Salaam.
 
Mwenyekiti wa zamani wa tawi hilo, Angel Akilimali akiendesha kikao cha uchaguzi

--
Umoja
Wanawake wa CCM, Tawi la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba
jijini Dar es Salaam, umefanya uchaguzi na kupata viongozi wapya.

Katika
uchaguzi huo, Mary Nchimbi ameibuka kuwa Mwenyekiti wa mpya wa tawi
hilo baada ya kupata kura 34 dhidi ya kura 28 alizopata mpinzani wake
Sheila Luckusasi.

Nafasi
ya Katibu wa tawi hilo ilikwenda kwa Naomi Daudi ambaye alijizolea kura
62 na kumwacha mbali mpinzani wake, Arafa Athumani aliyeambulia kura
mbili tu.

Katika
nafasi ya Ujumbe wa kuwakilisha Tawi kwenye ngazi ya wilaya ulikwenda
kwa Sheila Luckusasi ambaye baada ya kukosa Uenyekiti alifuta machozi
kwa kupata nafasi hiyo kwa taabu baada ya kumshinda mpinzani wake Zainab
Bwamkuu kwa kura moja kwa kupata kura 36 dhidi ya 35.

Pia
Selina Mbelwa naye aliibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha ujumbe wa
Halmashauri Kuu ya Tawi baada ya kujipatia kura 40 dhidi ya 30
alizopata mpinzani wake Jeni Mafinga.










0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa