Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKI PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO" YA BIA ZA SERENGETI

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKI PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO" YA BIA ZA SERENGETI



Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imewataka watanzania kushiriki kwa nguvu  zote katika promosheni ya Vumbua Hazina ya Chini ya kizibo ili kuweza kushinda zawadi mbali mbali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Masoko wa Kambpuni ya SBL, Ephrahim Mafuru  na
kusema kuwa SBL imetenga sh. Milioni 783 ambazo zitatolewa kama zawadi
kwa washindi wa promosheni hiyo ambayo itafanyika kwa wiki 16 kuanzia
Aprili 22.
Mafuru
alisema kuwa zawadi kwa wale watakao jishindia zawadi ya bia zina
thamani y ash. Milioni 265 zawadi za fedha taslim ni sh. Milioni 383.
Alisema kuwa pia watatoa pikipiki 16, Bajaj inane (8) , Jenereta nane
(8) na magari matatu aina ya Ford Figo.
 Alisema kuwa ili kuweza kuingia katika shindano hilo unatakiwa kununua bia zao, Serengeti, Tusker au Pilsner  na kukuta neno  lenye tarakimu saba na kulituma kwenda namba maalum ya 15317 na kuingia katika shindano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile, Freddie Manento aliipongeza SBL kwa
kuiteua kampuni yake kuendesha shindano hilo hasa kwa kuzingatia ubora
wa huduma zake.
Manento alisema kuwa kampuni yao ni bora zaidi katika kuendesha zoezi kama hilo na kuahidi kutoa hudima bora kwa wateja wake.
“Ni
faraja kubwa kufanya kazi na SBL katika shindano hili kubwa la
kuwazawadia wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ya bia,
tutafikisha lengo lililowekwa,” alisema Manento.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa