Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC) kuzinduliwa kesho

Jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC) kuzinduliwa kesho

 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)kama linavyoonekana pichani litakalozinduliwa tarehe 29 mwezi huu,Jengo hili litatumika kama kitega uchumi wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki ya Pwani.
 Mchungaji wa usharika wa kijitonyama Ernest Kadiva akifafanua jambo kwa wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la kitegauchumi cha usharika huo litakalojulikana kama KIJITONYAMA LUTHERAN CENTRE(KLC) litazinduliwa jumapili tarehe 29 mwezi huu,Ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka 2009 na kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 3.5.
 Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Dayosisi ya Usharika wa Kijitonyama Dkt.Hans Macha kulia akisisitiza jambo kwa Katibu wa Kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)Bw.Leonard Shayo ambalo litatumika kama kitega uchumi wa kanisa hilo,Baada ya kumaliza mkutano  na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwafahamisha juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.

 Katibu wa baraza la kanisa hilo Dkt.Victoria Kayombe akiongea na baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)litakalotumika kama kitega uchumi wa kanisa hilo,mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu,wa pili kutoka kushoto Mchunga wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva,Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi Selina Mkony,Mzee wa baraza la kanisa Leonard Shayo na Mjumbe wa kamati hiyo Peniel Uliwa.Ujenzi huo umegharimu kiasi cha Bilioni 3.5
 Katibu wa baraza la kanisa hilo Dkt.Victoria Kayombe akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa Jengo la Kijitonya Lutheran Centre(KLC)litakalotumika kama kitegauchumi wa Kanisa hilo,Jengo hilo litazinduliwa rasmi Aprili 29,katikati Mchungaji wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva na Mwenyekiti wa ujenzi Bw.Sanyiel Kishimbo.
Baadhi ya  wanakamati wa maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)walioudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya uzinduzi wa Jengo hilo litakalozinduliwa Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa