Home » » KIPINDI KINACHOPENDWA SANA TANZANIA ‘DALADALA’ SASA KINAITWA ‘MINIBUZZ’ CHARUSHWA HEWANI NA TBC!

KIPINDI KINACHOPENDWA SANA TANZANIA ‘DALADALA’ SASA KINAITWA ‘MINIBUZZ’ CHARUSHWA HEWANI NA TBC!




Mark Zuckerman mtayarishaji wa kipindi cha Mini Buzz akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika ofisi za kampuni ya R&R jijini Dar es salaam leo, kutoka kulia ni Tumaini Meskack mtangazaji, Christina Mbunda Mtangazaji na Daniel Kijoh Mtangazaji wa kipindi hicho

Watayarishaji maarufu wa kipindi cha runinga cha ‘daladala’ leo
wamezindua upya kipindi hiki kwenye televisheni ya TBC kikiwa na jina jipya la
Minibuzz.

Minibuzz ni kipindi kinachoatayarishwa na MADE IN AFRICA TV, kampuni ya utengenezaji na utayarishaji wa vipindi
ambavyo vina ujumbe kwa ajili ya jamii ya kiafrika.. 

Awali kilizinduliwa hapa nchini Tanzania mwaka 2010, kama daladala na
kwa muda mfupi sana kilipata wapenzi wengi takribani watu milioni tatu.   Na kwa
mafanikio hayo, kampuni hiyo iliweza kuzindua mfumo huo huo katika nchi ya
Uganda na Kenya.

Mtayarishaji mkuu, Frank Bierens, alisema,
“Jina lipya la
Minibuzz linakusudia kuongeza nguvu na kuunganisha Afrika mashariki.  Kwa kufanya kazi chini ya jina moja na
kushirikiana katika utayarishaji, kwa hivyo tunatarajia  kuepukana na usumbufu katika soko na kuwa
wazi kwenye makusudio ya kipindi hiki”. 

Minibuzz inarekodiwa kila asubuhi ndani ya gari ndogo aina ya Hiace
ambayo ina muundo wa studio.  Ina camera,
vinasa sauti na vifaa kwa ajili ya uhariri.
Washiriki ni abiria wa kawaida ambao hupanda basi hili katika vituo
mbalimbali nchini kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali yanayohusu maisha
yao. 


Daniel Kijoh akitoa maelezo kuhusu kipindi hicho.

Kipindi hiki chenye jina jipya kitaendelea na watangazaji wake Daniel
Kijo na Bibi
Kiroboto sasa hivi kina
sura mpya kabisa ya Tumaini Meshack.


Watayarishaji wa vipindi wa MADE IN AFRICA TV –wametangaza uzinduzi wa
kipindi cha Radio cha
Minibuzz kitacholetwa
kwenu na Bibi Kiroboto akishirikia na
Daniel
Kijo na Tumaini Meshack. Mfumo huu mpya unakusudia kuleta mwamko kwa wapenzi na
wasikilizaji nchini.

Daniel Kijo amesema, “Nina furaha kubwa kwa kuzinduliwa kwa kipindi
hiki, kama awali hii ni nafasi ya mtu wa kawaida kabisa kusikika na kuleta
changamoto ya mabadiliko Tanzania.
Katika mabadiliko ya kipindi hiki, tunatarajia kuwafikia na
kuwaunganisha watanzania wengi zaidi.    Kwa
kufanya vipindi vya televisheni na Radio tunaleta muungano katika mipaka yote
ya kijamii Tanzania.



Tumaini Meshack ambaye ni mtangazaji mpya wa
kipindi cha Minibuzz amesema, ”Nimefurahi kuungana na timu hii ya Minibuzz kwani
kwa muda mrefu nimekuwa mpenzi wa kipindi hiki.
Na sasa, tunatarajia kuungana na watazamaji wetu wote, katika mada
tofauti muhimu za kila siku.  Ni kupitia
mazungumzo au mijadala, tunaweza kuendeleza na kuboresha hali ya maisha hapa
Tanzania


Waandishi wa habari wakipanda kwenye gari linalotumika kuendesha kipindi cha Mini Buzz.

Akiongezea yaliyosemwa na wenzake, Bibi
Kiroboto naye alikuwa na haya ya kusema, “Mimi nimefurahi zaidi kwa kipindi cha
radio cha Minibuzz kwa vile tutawafikia watanzania wengi zaidi hususani
vijijini. Radio inaikika kila sehemu na wakati wowote. 

Kipindi cha Minibuzz cha televisheni kinarushwa hewani kila siku
katika televisheni ya TBC1 saa kumi na mbili jioni.   Kwa
redio, ni kila siku saa moja jioni katika kituo cha radio cha TBCFM.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Ms. Eugenia Chanda kwa
simu namba 0713 548496. Au kwa barua pepe, eugeniachanda@yahoo.com

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa