Home » » MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS

Mama Salma Kikwete Mke wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya STAND UP FOR AFRICAN
MOTHERS iliyoandaliwa na AMREF ambapo aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano wa kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto wao
wakati wa kujifungua, Mama salma alisema kuwa kila mwananchi akichangia
Sh.1000 za kitanzania, zitasaidia kusomesha wakunga 4222 watakaotumika
kuwauguza wamama wajawazito pindi wanapokuwa kwenye kipindi cha
kujifungua, Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja 
jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Dk Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi
huo ambapo aliitaka Amref isaidie kukusanya pesa kutoka kwa nanchi
pamoja ana Makampuni Binafsi ili fedha za kusomesha wakunga zipatikane.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Amref wakisherehekea kwenye uzinduzi huo.
Mama Salma Kikwete akimpongeza Mkurugenzi mkuu wa Amref Dk Festus Ilako kwa kuonyesha upendo kwa kinamama wajawazito.
Kikundi cha Burudani kutoka Mjomba Band kikifanya mambo kwenye Uzinduzi huo.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa